Maria Said mama
mkubwa wa Nasra, katikati ni baba mzazi wa Nasra, Rashidi Mvungi, na kulia ni
mume wa Mariam Said wakiwa katika ofisi za ustwawi wa jamii mjini Morogoro baada
ya kukamatwa na kufikishwa polisi kwa tuhuma za kumficha mtoto huyo ndani ya
box kwa miaka 4 baada ya mama wa mtoto huyo kufariki dunia kwa ugonjwa wa
malaria .
Muuguzi katika Wodi
ya watoto hospitali ya rufaa ya Morogoro akimuhudumia mtoto Nasra Said mara
baada ya kufikishwa hopsitalini hapo kupatiwa
matibabu.
Mtoto Nasra akiwa katika wodi ya watoto hospitali ya
mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu kwa sasa.
Habari zaidi
soma hapo chini.
MUME na mke
wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumficha mtoto kwa miaka 4
ndani ya Box .
Kamanda wa polisi mkoani
Morogoro Leonard Paul alisema tukio hilo lilibainika Mei 20 mwaka huu majira ya
saa 4.45 Asubuhi katika eneo la mtaa Azimio kata ya Kiwanje Ndege
Morogoro.
Alisema majirani
walizingira nyumba ya mwanamke ajulikanae kwa jina la Maria Said na kutaka
kuvunja ndipo polisi walipopata tarifa na kufika katika nyumba hiyo na kukuta
mtoto huyo akiwa katika box.
Alimtaja mtoto huyo
aliyejulikana kwa jina la Nasra Rashid Mvungi mine na nusu ambapo polisi
ilichukua jukumu la kupeleka kesi hiyo Ustawi wa jamii ili kuendela
nayo.
Afisa Ustawi wa jamii
katika ofisi ya mkoa wa Morogoro Oswing Ngungamtitu alisema mtoto huyo
alipelekwa hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa sababu alionekana kuwa na
afya dhoofu.
Alisema alilazwa na
kwamba kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa ustawi wa jamii huku wakiwachukulia
hatua za kisheria walezi wa mtoto huyo Mariam Said na Mume wake Mtonga
Omari.
Baba mzazi wa mtoto huyo
alisema yeye ana mke na watato wengine wa ndoa na kwamba hakuwahi kumwambia
mkewe kama ana mtoto wa nje hivyo ilikuwa vigumu kumchukua mtoto huyo na ndipo
alipomkabidhi mama mkubwa wa mtoto huyo.
Alisema kila mara alikuwa
akifika kumwona mtoto mama huyo alimwambia mtoto kalala na hivyo kushindwa
kumwona na kujua hali halisi hadi siku ya tukio na kwamba alikuwa akimpatia
matumizi ya mtoto huyo.
Ofisa mtendaji wa kata
hiyo Dia Zongo alisema akiwa katika kazi za kawaida katika Mtaa wa Azimio,
alipata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mwanamke huyo, alimficha mtoto Nasra
ndani ya boksi na kwamba hamfanyii usafi wala kumtoa nje.
Zongo alisema baada ya
kupata taarifa hizo, alimtafuta Mwenyekiti wa mtaa huo, Tatu Mgagala na
kuongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo na kuanza kumhoji mwanamke huyo ambaye
alikuwa akijibu kwa kubabaika na kushindwa kueleza ukweli juu ya kuwepo kwa
mtoto huyo.
Zongo alisema wakati mtuhumiwa akiendelea kujibu maswali,
ghafla mtoto huyo alipiga chafya na kuanza kukohoa hali iliyowapa wasiwasi na
kuamua kuingia chumbani kwa mwanamke huyo kwa nguvu na kumkuta mtoto Nasrah
akiwa ndani ya boksi nyuma ya mlango .
Ofisa mtendaji huyo
alisema wakati wakimtoa mtoto huyo kutoka ndani ya nyumba ya mama yake huyo
mkubwa, ghafla kundi kubwa la watu waliokuwa na fimbo na mawe, walianza
kumshambulia mwanamke huyo, kitendo kilichomlazimisha (mtendaji) kutoa taarifa
polisi.
Baada ya kufikishwa katika kituo cha polisi mwanamke huyo
alikiri kuanza kumlea mtoto huyo tangu akiwa akiwa na umri wa miezi tisa na
kwamba hatua hiyo ilikuja baada ya mama yake, kufariki dunia mwaka
2010.
Mtuhumiwa huyo alisema
kwa mara ya mwisho, alimuogesha mtoto huyo Julai mwaka jana na kwamba alikuwa
akimwekea chakula na maji ndani ya boksi lililokuwa limewekwa nyuma ya mlango wa
chumba cha mwanamke huyo.
Hores Isaack Msaky Dk Mshauri wa watoto katika hospitali
ya mkoa wa Morogoro alikiri kumpokea mtoto huyo na kwamba tayari ameshaanzishiwa
matibabu ya awali .
‘’ Tulimfanyia vipimo vya awali mtoto amebainika kuwa na Nimoni
pamoja na utapia mlo na sasa ameshaanza matibabu’’ Alisema
Alisema bado wanaendela
na vipimo vingine vya XRay kubaini mtoto huyo alipata ulemavu kwa kupigwa au
alizaliwa hivyo.
Alisema mtoto huyo
anamaumivu makali sehemu ya mgongo na mikono na kwamba mwili wake pia ni mteke
kama wa mtoto mchanga hali inayowafanya kuendela kumfanyia uchunguzi wa kina
zaidi.
Baadi ya mashuhuda wa
tukio hilo walidai kuwa mama wa mtoto huyo alifariki dunia miaka mine iliopita
na kwamba Mariamu Ni mama mkubwa wa mtoto huyo.
Hata hivyo majirani
hao walidai wanahusisha tukio hilo na imani za kishirikina kutokana na kwamba
mama huyo anaakili timamu na analea watoto wake vema tofauti na mtoto
huyo.
0 comments:
Post a Comment