Wateja wa Airtel kununua Tiketi za Ndege za Precicsion Air
kupitia huduma ya Airtel Money
· Wateja wa Airtel wawezeshwa kulipia tiketi zao za ndege kwa
njia rahisi na haraka zaidi
Dar
es Salaam Jumatano , Mai 14, 2014, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
imeanzisha ushirikiano na Precision Airtel utakaowawezesha wateja wake nchi
nzima kununua tiketi za ndege kupitia huduma ya Airtel
Money.
Ushirikiano
huu utawapatia wateja wa Precision Air urahisi katika kupanga safari zao na
kuwawezesha kununua ticket zao wakati wowote bila usumbufu kupitia huduma ya
Airtel Money.
Akionge
wakati wa uzinduzi Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema “ushirikiano huu utawapatia wateja wetu wa
Airtel njia mbadala, rahisi naya uhakika ya kulipia safari zao za ndani na za
nje huku ikiwapatia watanzania na wateja wetu uzoefu tofauti wa kufanya malipo
ya tiketi zao za ndege kupitia simu zao za kiganjani. Kwa kupitia huduma hii
mpya sasa wateja wetu wataweza kufanya malipo ya tiketi zao za ndege mahali
popote kwa usalama na haraka zaidi kupitia huduma ya Airtel Money.
”
“Tutaendelea
kuthibitisha dhamira yetu ya kutoa bidhaa na huduma za kibunifu huku
tukiwahakikishia wateja wetu huduma bora kupitia huduma ya Airtel Money na
nyinginezo wakati wote”. Aliongeza Matinde.
Akiongelea
kuhusu ushirikiano huo Afisa Masoko wa Precision Air Bwana Hillary Mremi alisema
“ ushirikiano huu umekuwa kwa wakati muafaka wakati Precision Air imejipanga
kuboresha huduma zetu na kuwapatia wateja wetu uzoefu tofauti katika huduma za
ndege huku tukihakikisha wateja wanafurahia huduma zetu zinazoenda zaidi ya
matarajio yao.
Wateja
wetu sasa wanaweza kufanya malipo ya tiketi zao za ndege kwa kupitia huduma ya
Airtel Money . kupitia simu zao za mkononi wateja wetu wanaweza kupiga call
center au kutembelea tovuti yetu kufanya booking ya safari zao na kulipia
kupitia Airtel Money na kisha kupokea tiketi yako kupitia simu yako ya mkononi”
aliongeza Mremi.
Akiongea
kuhusu namna ya kupata huduma hiyo Meneja uendeshaji wa Airtel Money Asupya
Naligingwa alisema” huduma hii ni rahisi kutumia , mteja anachotakiwa kufanya ni
kupiga simu na kufanya booking ya safari au kufanya booking kupitia tovuti ya
Precision Air ambapo mteja atapewa namba ambayo itatumika kama reference wakati
wa malipo.
Kununua tiketi kupitia Airtel Money wateja wanatakiwa kufanya
yafuatayo
Piga
*150*60#
|
Chagua namba 5 (Lipia
Bili)
|
Chagua namba 8
(NYINGINEZO)
|
Andika
jina la biashara
|
PW
|
Ingiza
Kiasi cha pesa
|
Kumbukumbu
rejea
|
(namba
ya booking)
|
Ingiza neno la siri kulipa PW, Tsh xxxxx,
kumbukumbu rejea namba
xxxxxx
|
Baada
ya kufanya hayo utapokea ujumbe wenye uthibitisho wa malipo na tiketi yake ya
ndege “aliongeza Nalingingwa.
Huduma
ya Airtel Money ni huduma inayowawezesha wateja wa Airtel Nchi nzima kufanya
malipo na miamala ya pesa kupitia pesa simu ya mkononi . kwa kupitia huduma ya
Airtel money wateja wanaweza kulipia ankra kama vile DAWASCO, LUKU, USA visa,
DSTV, kulipia mikopo , kununua muda wa maongezi, kununua vifurushi vya yatosha
na kutuma na kupokea pesa kutoka kwa marafiki na familia na huduma nyingine
nyingi.
0 comments:
Post a Comment