NYOTA wa zamani
wa Manchester United, Roy Keane amemuonya Phil Jones kuwa anahitaji kugangamala
kama kweli anataka kuwa mchezaji tegemeo Manchester United.
Jones
alichukuliwa kama Duncun Edwards (beki nyota wa zamani wa United) wakati
aliposajiliwa kwa pauni milioni 16.5 kutoka Blackburn Rovers mwaka
2011.
Lakini Keane
amedai beki huyo amepoteza muda mwingi kwa kuwa majeruhi kama alivyo mchezaji
mwenzake Chris Smalling aliyesajiliwa mwaka 2010 kutoka Fulham kwa pauni milioni
10 ambaye Roy Keane anasema maendeleo yake yamekuwa yakirudi nyuma siku hadi
siku.
Keane alisema:
“Tuliambiwa Jones atakuwa Duncan Edwards – Smalling atakuwa hivi na
vile.
“Nimetazama
‘live’ mechi kumi za United mwaka huu na wamekuwa hawana cha kufanana na hayo
yaliyosemwa juu yao. Kama kuna chochote basi nadhani ni kwamba wamekuwa
wakiporomoka.
“Unasema
unapaswa kuwapa wachezaji nafasi ili wakomae, lakini pia unakuwa na wachezaji
ambao utawaambia, ‘Umepewa nafasi na umeshindwa kuitumia’. Wanapaswa kuongeza
kiwango chao kama kweli wanataka kuwa nyota wa Manchester United.
“Jones
anahitaji kugangamala. Kila wakati nimekuwa nimekuwa nikiumuona akitolewa nje
kwa kuumia.”
Roy Hodgson
amewachukua wachezaji wote hao wawili kwenye kikosi cha timu ya taifa cha
England kitakachokwenda Brazil Kombe la Dunia wakitarajiwa kuwa suluhisho la
mabeki wa kati iwapo Gary Cahill na Phil Jagielka watakuwa hawako
fiti.
Alipoulizwa
kama wachezaji hao ni wazuri kiasi cha kuwa mbadala wa mabeki wa kati, Keane
aliongeza: “Sio kwa kiwango chao cha sasa. Wawili hao wamekuwa na msimu
mbovu.
“Lakini pengine
England inaweza ikawahitaji, unaweza ukawa na majeruhi. Pengine kwenye nafasi
zingine wanaweza wakahitajika. Labda hiyo ndio sababu kubwa ya Roy kuwachukua
Jones na Smalling, kwa kujua kuwa wanaweza kucheza hata kama mabeki wa pembeni
au kiungo.”
0 comments:
Post a Comment