July 09, 2014

  • MH. MAKALLA AFANYA ZIARA JIMBONI KWAKE MVOMERO



    MH. MAKALLA AFANYA ZIARA JIMBONI KWAKE MVOMERO
    Na John Nditi, Morogoro

    Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ,ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji,kuanzia Julai 3 hadi 7, mwaka huu, alifanya ziara ya kikazi iliyilenga kuhamasisha shughuli za maendeleo ya wananchi wake wa vijiji mbalimbali vya Tarafa ya Mlali, Turiani na Mvomero.

    Katika ziara hiyo, ametoa misaada ya aina mbalimbali ya kifedha na vifaa kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na kuzundua vituo vya kuchota maji Kijiji cha Mgogo, Kata ya Sungaji, Kijiji cha Mlali na Kipera, kutoa misaada ya kifedha kwa vikundi vya akina mama wajasiliamali, vijana , taasisi za dini na ujenzi wa ofisi za CCM kata na Matawi.

    Sehemu kubwa ya misaada ya kifedha ilielekezwa kwenye sekta ya elimu katika kusaidia uendelezaji wa ujenzi majengo ya madarasa la shule za awali na mikondo ya darasa la kwanza kwenye vijiji vilivyopo kwenye Tarafa hizo kufuatia wananchi kuonesha nguvu zao wakiwa na lengo la kuwaondolea adha watoto wao wanaotembela umbali mrefu kwenda shule.

    Mbunge hiyo pia akiwa Mji Mdogo wa Dakawa, alikabidhi msaada wa vyakula kwa kutoa tende katoni 50 na mchele tani 1.5 kwa ajili ya waumini wa dini ya kiislamu ambao wapo kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan wilaya huo.
    Baadhi ya wanawake wa vikundi vya vicoba wakimsikiliza mbunge wao (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara eneo la Dakawa.
    Kazi imeenda vizuri,msimamizi wa mradi maji akimnong'oneza Naibu Waziri wa Maji ambaye ni Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla (mwenye shati la kitenge).
    Kuwafikia wananchi wa kutumia njia ya miguu sehemu ambako hakuna daraja la kupita magari.
    Mbunge Amos Makalla ambaye ni Naibu Waziri wa Maji, akimtwisha mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Mlali ndoo ya maji baada ya kuzindua kituo cha kuchota maji.
    Mbunge Amos Makalla,wenye suti akizungumza na viongozi wa dini ya kiislamu wa kijiji cha Pemba ili kuona namna ya kusaidia ujenzi wa msikiti.
    Mbunge wa Jimbo la Mvomero akiwa pamoja na wananchi wake wa jamii ya kimasai eneo la Kitongiji cha Nyakonge.
    Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makall akilisiliza utenzi.
    Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla akishika gunia la mchele pamoja na mmoja wa mashehe wa Kata ya Dakawa, alipokabidhi tani 1.5 za mchele na tende boksi 50 kwa waislamu waliofunga mwezi mtukufu wa ramadhani.
    Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mvomero, Abdallah Mtiga (kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo hilo, Amos Makalla,ambaye ni Naibu Waziri wa Maji, kabla ya kuwahutubia wakazi wa Dakawa.
    Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mvomero, Abdallah Mtiga akitoa neno kabla ya kumkaribisha Mbunge wa Jimbo hilo, Amos Makalla ,(kaunda suti) Kijiji cha Kidudwe, kwenye utekelezaji wa mradi wa uchimbaji kisima kirefu cha maji.
    NAIBU WAZIRI WA MAJI, AMOS MAKALLA NA CHAI YA ASUBUHI NA JAMII YA KIMASAI.
    Shehe Juma Munga wa Msikiti wa  Kijiji cha Kobogoji ,Kata ya Kibati,wilayani Mvomero akiendesha dua ya kumwombea heri Mbunge wao.
    UMATI WA WAKAZI WA DAKAWA WAKI.
    Utekelezaji wa Ilani ya CCM kuhusu huduma za maji safi na salama vijijini.
    Viongozi wa Jumuiya za CCM Wilaya ya Mvomero wakiserebuka.
    WANAKWANYA WA KITONGOJI CHA NYAKONGE,KIJIJI CHA PEMBA WAKIIMBA MBELE YA MBUNGE WAO.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.