Mbunge
wa zamani wa jimbo la Kwela, Mzee Chrisant Mzindakaya (shoto) amekataa
kumsamehe hadharani Mbunge wa sasa wa Sumbawanga Mjini, Bw. Aeshi Hilali
(kulia) baada ya kupewa fursa ya kushikana mikono jukwaani na
kusameheana.
Haya yametokea leo mchana (Jumapili, Mei 25, 2014) kwenye ibada ya kumuweka wakfu Askofu Mteule Conrad Nguvumali wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Rukwa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga.
Haya yametokea leo mchana (Jumapili, Mei 25, 2014) kwenye ibada ya kumuweka wakfu Askofu Mteule Conrad Nguvumali wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Rukwa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga.
Mzee
Mzindakaya alikataa kufanya hivyo akisema yeye ni mkristu lakini hakuwa
ameandaliwa kiroho kwa ajili ya tukio hilo. “Hapa ni shughuli ya kanisa
na si mkutano wa Chama. Lazima niwe mkweli leo sijajiandaa kwa jambo
hili… Mimi ni mtu mzima, nafsi ya msamaha inahitaji maandalizi, nahitaji
maandalizi ya kiroho,” alisema.
Hata
hivyo, alikiri kwamba amekubali msamaha alioombwa na Bw. Aeshi lakini
hawezi kuutoa katika shughuli ya Kanisa. “Nilishamwambia Mwenyekiti wa
CCM mkoa aitishe mkutano, wazee wa chama wawepo na sisi wawili tuwepo
kwa sababu nimetukanwa sana kama vile sijaifanyia jambo lolote nchi
hii,” alisisitiza.
“Niliwaeleza
pia waandae mikutano ya nje kule kwa wanachama ambako nilichafuliwa
sana. Nikisema nimemsamehe hapa nitakuwa mnafiki,” aliongeza.
Kwa
upande wake, Bw. Aeshi ambaye alipewa nafasi ya kwanza kuomba msamaha,
alisema anatambua kwamba bega haliwezi kukizidi kichwa na yeye kama
mtoto anamuomba msamaha Mzee Mzindakaya kwa yaliyopita ili waweze
kufanya kazi pamoja na kuleta maendeleo kwa wakazi wa jimbola Sumbawanga
Mjini.
“Natambua
kuwa mimi ni mtoto na siku zote mdogo atabaki kuwa mdogo lakini naomba
busara zake ili tushirikiane kuleta maendeleo ya mkoa wetu… yaliyopita
si ndwele tugange yajayo. Nimetamka maneno haya mbele ya viongozi wa
dini na mbele ya Mungu kwa kuwa najua yuko hapa,” alisema.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya ndiye aliwaomba Mzee
Mzindakaya na Bw. Aeshi wapande jukwaani na kupeana mikono na kisha
akawapa kila mtu fursa ya kutoa neno.
Mhandisi
Manyanya alisema siku ya leo ni ya kipekee na akaona asipoteze fursa
hiyo bali aitumie kuwaomba viongozi hao ambao wamekuwa na uhasama wa
muda mrefu wayamalize kwa kupeana mikono hadharani.
0 comments:
Post a Comment