WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda (pichani) amesema Serikali itaendelea kusimamia
msimamo wake wa kutokuwa na dini wala nchi kutokuwa na dini lakini
itaendelea kuruhusu watu wawe na dini zao.
Ametoa
kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Mei 25, 2014) kwenye ibada ya kumuweka
wakfu Askofu Mteule Conrad Nguvumali wa Kanisa la Moravian Tanzania
Jimbo la Rukwa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mjini
Sumbawanga.
Waziri
Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ambaye
yuko nje ya nchi kikazi, alisema: “Leo tukiruhusu Serikali iwe na dini
na tayari katika dini zote kuna makundi madogo madogo, je wale wa upande
mwingine utawaacha wapi?”.
Pia
alitumia fursa hiyo kuwaasa viongozi wa dini nao pia waangalie
wasitumbikie kwenye mtego wa siasa na kuruhusu kanisa zima liwe la chama
fulani kwani miongoni mwa waumini wao wapo pia wapenzi wa vyama
vingine.
“Kama mtu binafsi, kiongozi wa dini anaweza kuwa mpenzi wa chama lakini kama Kanisa tusiruhu hali hiyo,” alionya.
Aliwaomba
viongozi wa dini waendelee kuliombea Taifa na hasa waombee amani ya
Taifa hili. “Ninawasishi viongozi wa dini msichoke kuombea amani ya
Taifa hili kwani amani ikipotea kama nchi hatuna mahali pa kukimbilia.
0 comments:
Post a Comment