Umati wa watu ukiwa
unashangaa kitendo cha mwanadada (kushoto mwenye kitambaa cha zambarau
kichwani) aliyemkwapulia
20,000
mwenzake.
MWANADADA mmoja ambaye
jina lake halikufahamika amejikuta akinusurika kupigwa na wananchi wenye hasira
kali baada ya kumuibia mama aliyekuwa na mtoto.
Ishu nzima imetokea
maeneo ya jirani na hospitali ya Amana, Ilala, jijini Dar es Salaam, ambapo
baada ya mama mmoja aliyekuwa na mtoto kumkabidhi mwanadada (mwizi) mtoto na
mkoba wake, ndipo mdada huyo alipochomoa shilingi 20,000/= kwenye mkoba wa mama
huyo.
Aliporudi mama wa mtoto
alimkabidhi mtoto na mkoba wake kisha kuondoka kwa haraka na wasiwasi mwingi,
kitu kilichomshitua yule mama na kujisachi ndipo alipobaini kuibiwa na kuanza
kupiga kelele za mwizi.
Vijana walionyesha uwezo
wao kwa kumkimbiza na kumkamata ambapo alinyang’anywa pesa na zogo likaibuka
wakati wengine wakitaka kumpiga huku baadhi ya vijana wakionekana kumkingia
kifua kwa kuwa ni mwanamke.
0 comments:
Post a Comment