May 14, 2014

  • MBARONI KWA KUWAHIFADHI WAHAMIAJI HARAMU GEITA.



    Idara ya uhamiaji mkoani geita inawashikilia watanzania wawili wakazi wa Nyamboge wilayani Geita kwa tuhuma ya kuwahifadhi nyumbani kwao wahamiaji haramu 18 kutoka nchini Burudi kinyume cha sheria
    Afisa uhamiaji Mkoa wa Geita kamishina msaidizi mwandamizi wa idara hiyo Charles Washima amesema watanzania hao walikamatwa jana wakiwa pamoja na wahamiaji hao waliokuwa wakiwatumikisha shughuli za kilimo cha mananasi
    Washima amesema watanzania hao ni Masumbuko Mihangwa (34) na Japheth Kwilukilwa (27) wanatuhumiwa kuwakaribisha wahamiaji hao kinyume cha sheria na kuwaajili katika mashamba yao katika maeneo ya Nzera, Katoma na Nyamboke ambao walikuwa wakifanya vibarua
    Kufatia hali hiyo Washima amesema  taratibu za kuwafikisha mahakamani watanzania hao pamoja na wahamiaji hao kutoka nchini Burundi zinaenderea huku akiwataja baadhi yao ni Saimon Hakizimana, Nkuluzinza Elize pamoja na Shitete Meshack

    Aidha Washima ametaja wahamiaji wengine ni pamoja Abedi Sijali, Edward  Rashid,  Mahirambwa Siliveli, Kahonalikie Paschal pamoja na Mwiluluko Paschal ambapo amewataka wananchi mkoani Geita kuacha mara moja  tabia ya kukaribisha wahamiaji haramu bila kuogopa mkono wa sheria
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.