May 21, 2014

  • Mwanafunzi azimia na kupoteza Fahamu baada ya kubakwa na watu wasiofahamika nyumbani kwa bibi yake

     
     
     
     

    Mwanafunzi  wa Shule ya Msingi Liami wilayani Ifakara mkoani Morogoro (jina limehifadhiwa), amebakwa na watu wasiojulikana alfajiri ya Mei 5, mwaka huu nyumbani kwa bibi yake.


    Akizungumza na Uwazi, mama wa binti huyo mwenye umri wa miaka 13, Neema Ally akiwa wodi A ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alisema mtoto wao alienda nyumbani kwa bibi yake kulala baada ya kumaliza kula kwa wazazi wake.
     
    Alisema watu waliofanya unyama huo, pia waliiba baiskeli kabla ya mtoto wao kuokolewa na wasamaria wema waliosikia mayowe yake ya kuomba msaada ambapo walimkuta akitokwa na povu mdomoni.
     
     
    Alisema wasamaria wema hao walimkuta mtoto wake akiwa amepoteza fahamu kutokana na kukabwa koo wakati akifanyiwa kitendo hicho.
     
    "Hali ilipozidi kuwa mbaya alipelekwa Hospitali ya St. Frances, Ifakara ambako nako hakukaa, akahamishiwa hapa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
     
     
     
    "Ilimchukua muda wa siku tatu mtoto kupata fahamu, nawashukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara kwa  kutoa  gari la kubebea wagonjwa kwa haraka ili kunusuru maisha ya mwanangu na fedha," alisema Neema.
     
    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.