Ripota wa nguvu Simon Simalenga akiwa 104.4 Dodoma amekutana na Wanachuo kwenye chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo kwenye bunge la bajeti linaloendelea May 19 2014 Wabunge walipitisha bajeti ya wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ambayo ni Bilioni 799.2
Ndani ya saa 24 toka kupitishwa kwa bajeti hiyo taarifa zinapatikana kwamba kuna uwezekano wa kutokea maandamano ya Wanachuo wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kuelekea bungeni kama hawatopata fedha zao za kujikimu ambazo wamecheleweshewa kwenye collage yao ya Humanities.
Wanasema 'hatujazungumza hivi sababu tumepanic, kikawaida chuoni tunatakiwa kusaini boom kila baada ya siku 56 ambazo ziliisha 26 April 2014 na mpaka hatujapata taarifa yoyote toka wakati huo kwamba kuna shida gani imetokea'
Mwajuma Ally ambae ni Mwanachuo wa UDOM pia amesema 'niko mwaka wa pili, tunashindwa kuelewa kwa nini hili tatizo limetokea mpaka sasa hivi inaonekana sisi tunadharaulika manake hii ni mara ya pili inatokea humanities lakini vyuo vingine wamepewa mikopo'
Wengine wanasema 'Wanaume wenyewe sisi wapiganaji mpaka sasa tunaumia… watoto wa kike je?' Mwananchuo mwingine aitwae Upendo amesema 'hii kashfa ya watoto wa kike kujiuza kwa Wabunge ni ya kweli kwa sababu boom likichelewa ni bora nikakae maeneo ya bungeni kwa sababu nikimuelezea Mbunge nina shida nitalala nae atanipa hela'
'Ndio maana Wasichana wengi tunapenda kujiuza, sio kwamba tunapenda kufanya makusudi ila ni kwa sababu tunacheleweshewa hela na maeneo ya bungeni ndio tunapendelea kwenda kwa sababu tunajua kule ndio kuna mpunga mwingi kuliko sehemu nyingine'
Kwenye ofisi za utawala za chuo hicho Profesa Mbunda akatoa ufafanuzi kwa kusema 'kifupi ni kwamba management ya chuo kikuu inafatilia hilo swala, afisa wake wa juu kabisa wa mambo ya pesa yuko Dar es salaam na ameahidiwa katika siku tatu hili swala litakua limetatuliwa kwa hiyo tunaomba Wanachuo wetu wavumilie kwa siku tatu'.
0 comments:
Post a Comment