Na Woinde Shizza wa Globu
ya Jamii, Arusha
Zaidi ya machifu 100 kutoka
katika mikoa mbalimbali hapa nchini wanatarajia kushiriki katika tamasha la
"Mtu Kwao" linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi May 15 hadi 20 mwaka huu katika
kiwanja cha kumbu ya sheikh Amri Abeid jijini hapa.
Akiongea na waandishi wa
habari jijini hapa Mratibu wa tamasha hilo ambaye ni mkurenzi wa kampuni ya
Utamaduni Traning L.T.D Janeth Jonas alisema kuwa tamasha hilo litashirikisha
machifu 120 kutoka katika mikoa mbalimbali na makabila mbalimbali ya hapa
nchini.
Alibainisha kuwa nia na
dhumuni la kuandaa tamasha hili la mtamaduni wetu ni kuweza kuuenzi utamaduni wa
mtanzani ambapo ni kuanzia mavazi ya makabila mbalimbali,vyakula pamoja na ngoma
kutoka katika makabila yote hapa nchini.
“Pia katika tamasha hili
tumeamua kuwaita machifu mbalimbali l kutoka katika makabila mbalimbali hapa
nchini na baadhi ya mchifu ambao watauthuria ni pamoja na chifu kutoka oldmoshi
ambaye yeye ameshawasili hapa Arusha kwaajili ya tamasha hili Gerald Mandera
,chifu Gilbert Rugal Isambe kutok a kasulu na wengine wengi wote
watakuwepo”alisema Janeth
Aidha alisema kuwa katika
tamasha hili kila mtu atapata fursa ya kuona ngoma kutoka katika makabila
mbalimbali pamoja na kuonja chakula cha kila aina cha makabila ya hapa nchini
pamoja na nje ya nchi
Alisema kuwa pia katika
tamasha hili zaidi ya vikundi vya ngoma 100 vitatumbuiza pamoja na wasanii
mbalimbali akiwepo msanii wa ngoma za utamaduni Mrisho mpoto, Wema Sepetu, kundi
la Weusi kutoka Arusha, Jambo Squard, Dogo Janja pamoja na msanii kutoka nchini
Kenya Daniel ole Sekuo.
Naye mmoja wa machifu
ambaye atahudhuria tamasha hilo Chiefu Gerald Mandera kutoka Old Moshi alisema
kuwa waandaaji wamefanya jambo jema sana kuanda tamasha hili kwani wao ndio
wametambua uwepo wa machifu na wameona umuhimu wao mpaka wameamua kuwakusanya
pamoja katika tamasha kama hili.
Alisema kuwa sasa hivi
serikali nayo inawajibu wa kujipanga vilivyo na kutenga siku maalumu kwa ajili
ya kufanya tamasha hili kama jinsi wenzetu kutoka katika nchi zingine wanavyo
azimisha siku hii katika tarehe hizi na mwezi huu kila
mwaka.
Aidha alibainisha kuwa
kuwakusanya watu mbalimbali kutoka katika tamaduni mbalimbali pamoja na makabila
mbalimbali itasaidia kwani inaweza kuwezesha hata nchi kupata vazi la taifa
kwani makabila haya yate yanakuja yakiwa yamevaa vazi la ukabila wao na hii
itakuwa fursa pekee ya kuweza kuchagua vazi hasili la
mtanzanzia.
“Ni aibu kubwa sana
unakuta sisi kama Watanzania hadi leo hii hatuna vazi linaloweza kutuwakilisha
sisi kama Watanzania na ukiangalia wenzetu wa n je ya nchi wanamav azi yao ya
kiutamaduni ambao ukimuona tu mtu amevaa unajua katoka katika kabila Fulani
,naitanishangaza sana kuona mtu anauzarau utamaduni wake na anauweka mbele
utamaduni wa kigeni “alisema chifu Gilbert Isambe akibainisha kuwa hii ni fursa
ya watu kuja kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo
Chifu Gilbert Isambe akiwa na vazi la
kichifu
Chifu Gilbert Isambe
akiongea na vyombo vya habari. Pembeni yake ni mratibu wa tamasha la Mtu kwao
Bi. Janeth Jonas
0 comments:
Post a Comment