Muigizaji wa filamu mwenye jina kubwa nchini Jackline Wolper amesema kuwa watu wanaosema kuwa soko la filamu nchini limeshuka baada ya Kanumba kufariki ni waongo kwasababu kila mtu ana mashabiki wake na Kanumba hakuwa ameliteka soko peke yake.
Akizungumza katika The Sporah Show,Wolper alisema kuwa wanaosema hivyo itakuwa ni mashabiki wa Kanumba ndiyo maana baada ya kufariki wanaona soko limeshuka kwasababu walizoea kununua kazi zake....
"Unajua kuna mashabiki wa hivyo ambao wanaingia hata front kupigana ukimsema Wolper, ukimsema nani? sijui nani? you know, kwahiyo mimi ninaweza nikasema huyo ni shabiki yake sana Kanumba.
"Kwahiyo anaona Kanumba amekufa basi ndio kila kitu kimekufa. Kama juzi hivi nimefululiza kufanya movies kama tatu na Ray, wale ambao wanasema zimeshuka labda hawajapita madukani kuangalia lakini movies zipo nyingi tu"
0 comments:
Post a Comment