HOMA YA DENGUE NI NINI? Homa ya Dengue ni ugonjwa unaoenezwa kwa kuumwa na mbu aina ya Aedes mwenye virus vya ugonjwa huu. Mbu hupata virusi vya homa ya Dengue anapomuuma mtu mwenye ugonjwa huu. Ugonjwa huu unaenezwa kutoka mtu mmoja kwenda mwingine kwa kuumwa na mbu huyu. DALILI: Homa kali ya ghafla Kuumwa kichwa hususani sehemu za machoni Maumivu makali ya viungo na misuli ya mwili Kichefuchefu au kutapika Kutokwa na damu kwenye fizi, na sehemu za uwazi za mwili. Uchovu ukimsikia ndugu au jamaa yako anasema kuwa na dalili hizi muwahishe hospitali mapema. #SAMBAZA KUWASAIDIA NA WENGINE.
|
0 comments:
Post a Comment