BIBI
wa Kinigeria, Olabisi Ibidun Cole (65), leo ameangua kilio katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar ers Salaam wakati akipelekwa
kizimbani kwa ajili ya kusomewa kesi yake ya kunaswa na madawa ya
kulevya yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 37.
Hakimu
aliyepelekewa kesi hiyo, Frank Mushi, aliiahirisha kesi hiyo mpaka
kesho ili bibi huyo ambaye hajui Kiswahili wala Kiingereza atafute
mkalimani.
Cole
alisema lugha anayoweza kuitumia kiufasaha ni Kiyoruba ambacho hutumiwa
nchini Nigeria. Katika hali iliyoonesha kukata tamaa, bibi huyo alianza
kuangua kilio akiomba Mungu amsaidie.
0 comments:
Post a Comment