June 18, 2014

  • MISS TANGA 2014 WATEMBELEA MWAMBAO FM



    MISS TANGA 2014 WATEMBELEA MWAMBAO FM
    Washiriki wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 jana walitembelea kituo cha matangazo cha redio Mwambao Fm cha jijini Tanga kujionea jinsi kituo hicho kinavyorusha matangazo yake.

    Wakiwa katika kituo hicho, warembeo hao walipata fursa ya kuzungumzia shindano hilo huku kila mmoja akitamba kuibuka mshindi siku ya jumamosi ya tarehe 21/06/2014 ndani ya Mkonge Hotel kuanzia saa moja usiku.

    Baadaye leo washiriki hao watatembelea kituo cha redio cha Breeze Fm pia cha jijini Tanga na kesho wanataraji kwenda kutoa msaada katika moja ya vituo vya kulea watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

    Shindano hili limedhaminiwa na Nice & Lovely, EATV, Redd's, Tanga Beach Resort, Breeze Fm, CXC Africa, Rweyunga Blog na Mwambao Fm. Malkia wa mipasho Afrika Mashariki, Bi Hadija Omary Kopa ndiye atakayetoa burudani siku hiyo
    Washiriki wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakiwa wamelizunguka gari ambalo atakabidhiwa mshindi wa kwanza katika shindano hilo.
    Washiriki wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakiwa wamesimama mbele ya basi lao muda mfupi baada ya kutoka kutembelea kituo cha redio Mwambao Fm jijini Tanga.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.