Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa          Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares          Salaam leo.
        Baadhi ya          waandishi wa habari wakiwa kazini jijini Dar es Salaam leo.
        Na Magreth Kinabo 
        SHERIA mpya   ya Makosa ya Mtandao ya          mwaka   2015 na Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya mwaka 2015          zitaanza kutumika rasmi kesho Septemba Mosi mwaka huu, hivyo          watumiaji   na watoa huduma waaswa kuzingatia sheria hizi ili          kuepuka mkondo wa sheria.
         Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri          wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa          wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam          kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.
        "Sheria hizi ni nzuri zitaanza          kutumika Septemba Mosi mwaka huu,kuanzia saa 6.00 usiku . zina          maslahi katika nchi yetu. Ninatoa wito kwa wananchi kuzingatia          matumizi salama ya mtandao kwa manufaa yako na maendeleo ya          Taifa letu," alisema Profesa Mbarawa.
         Aliongeza kuwa sheria hiyo ya            makosa ya mtandao ya mwaka 2015 hazihitaji utungaji wa kanuni            kwa kuwa iko wazi.
            Alisema tayari wizara imeanza            kuelimisha watu kuhusu sheria hiyo na itendelea kuwajengea            uwezo wadau mbalimbali.
        Profesa Mbarawa alisema sheria ya          makosa ya mtando ya mwaka 2015 na Tanzania sio nchi ya kwanza          kuwa nayo, bali nchi mbalimbali zina sheria kama hiyo ,ambapo          alitolea mfano Uingereza,India,Malaysia, Uganda na Korea ya          Kusini.
        Akizungumzia kuhusu  madai sheria          hiyo kuhusika na suala la Uchaguzi Mkuu, alisema si kweli, bali          imekamilika katika kipindi hicho ndio maana baadhi ya watu          wanadai hivyo.Aliongeza kwamba sheria hiyo imetunga ili          kudhibiti matumizi ambayo  si mazuri. 
        " Mtu akitumiwa ujumbe akiupokea          hapaswi kuisambaza  kwani atakapousambaza atakuwa na amefanya          kosa,"alisisitiza.
        Aliyataja baadhi ya makosa kuwa ni          usiri, usalama wa upatikanaji wa taarifa za kompyuta na          mifumo  kama vilekuingilia mawasiliano ya kompyuta au mifumo ya          kompyuta kinyume cha sheria na wizi wa taarifa kimtandao.
        Makosa  dhidi ya kompyuta ikiwa ni          pamoja na,udanganyifu kwa kutumia kompyuta,kugushi kwa kutumia          kompyuta wizi wa utambulisho wa mtu binafsi  mtandaoni, matumizi          ya vifaa kinyume cha sheria
         Makosa yanayohusiana kimaudhui            kama vile usambazaji wa ponografia, ponografia za watoto            makosa dhidi ya ubaguzi wa rangi na chuki, michezo ya kmari            mtanadaoni kiunyume cha sheria, kashfa na habari za uongo na            makosa dhidi ya haki na hati miliki.
        Pia inatambua muungano wa makosa          inajumuisha kama vile utakatishaji wa fedha haramu na ugaidi kwa          kutumia mtandao.
        Kwa upande wa sheria ya miamala ya          kieletroniki ya mwaka 2015, baadhi ya makosa likiwemo la wajibu          wa watoa huduma kwa walaji, bidhaa ,huduma au mawasiliano ambayo          hayajaombwa na uhalali wa Muamala wa elektroniki.
        Aliongeza kuwa kanuni za sheria hiyo          zinatayarishwa zikiwa tayari zitangazwa  na zitaanza kutumika          wakati wowote.
        
0 comments:
Post a Comment