Baraza la taifa la usimamizi wa mazingira              {NEMC} limekifungia kiwanda cha Huwa Cheng Company Limited              kilichopo mjini Dodoma na kukitoza faini ya shilingi milioni              200 baada ya kubaini kiwanda hicho kinajihusisha na              usindikaji wa nyama ya Punda kinyume na utamaduni wa              watanzania huku mazingira yake yakiwa hatarishi kutokana na              uchafu unaozalishwa kuzagaa kwenye makazi ya watu.
                                                   
                          
        Ni                mabishano makali baina ya wamiliki wa kiwanda hiki raia wa                uchina na maofisa wa NEMC yaliyochukua muda mrefu kabla ya                maofisa hao kutoa tamko la kufungwa kwa kiwanda hicho                ambacho mbali na kuzalisha nyama ya Punda ambayo ni                kinyume na utamaduni wa watanzania lakini pia mazingira ya                uzalishaji wake ni hatarishi kwa afya za wafanyakazi na                majirani wa eneo hilo.
                        Kiwanda                hiki ambacho kwa siku kinadaiwa kuchinja Punda wasiopungua                200 inaelezwa kuwa mbali na kukiuka utamaduni lakini pia                kinaharibu kizazi cha wanyama hao ambao uzao wake unatajwa                kuwa ni mdogo hali inayotishia wanyama hao ambao kwa kanda                ya kati hutumiwa katika kazi mbalimbali kupungua ama                kutoweka kabisa.
            Mohamed                Hamis ni meneja msaidizi wa kiwanda hiki ambaye                anazungumza kwa niaba ya raia hao wa uchina anasema nyama                hizo za Punda zinasafirishwa kwenda kuuzwa nchini China.
            Sintofamahu                hii inaifanya ITV kuzungumza na wakazi wa mji wa Dodoma                ambao wanatupa lawama kwa mamlaka za mkoa kutobaini                kiwanda hicho na kukichukulia hatua huku kukiwa na taarifa                ya nyama hizo kuzagaa na kuuzwa katika maeneo mbalimbali                ya mji huo hasa kwenye mabaa na migahawa ya chakula.
            VIA-ITV
          
0 comments:
Post a Comment