MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na Mbunge wa Urambo aliyemaliza muda wake, Samuel Sitta ametaka uandaliwe mdahalo kwenye vyombo vya habari kati yake na mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa uelezwe ukweli juu ya ukweli wa sakata la Richmond.
          
Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge wakati Lowassa alipojiuzulu kutokana na sakata hilo, alisema katika mdahalo huo, ataeleza ukweli juu ya uhusika wa Lowassa katika sakata hilo na atatoa vielelezo kueleza taifa ufisadi uliokuwa ukifanyika.
          
Alisema hayo jana kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM mkoa wa Shinyanga katika mkutano uliofanyika mjini hapa ambao wagombea wa udiwani na ubunge wa majimbo yote ya mkoani hapa walitambulishwa.
          
Katika mkutano huo, alisema kujiuzulu kwa Lowassa mwaka 2008, kulitokana na Kamati Teule iliyoongozwa na Dk Harrison Mwakyembe, kugundua kwamba fedha za walipa kodi zilikuwa zikipotea bure.
          
Alisema yuko tayari kusimulia kwa              umma utajiri wa mgombea huyo wa Chadema. 
              
            Makundi, urafiki
            Sitta ambaye ni Waziri wa              Afrika Mashariki, ambaye pia alikuwa kwenye kinyang'anyiro              cha kutaka kuteuliwa kugombea urais kupitia CCM, alisema              wanamwamini Dk John Magufuli katika utendaji wake wa kazi na              pia ni kiongozi asiye na makundi au urafiki.
          
"Kweli lazima uwapime viongozi, kwani anayetaka urais lazima achaguliwe kwa kufuata utaratibu, achambuliwe usiogope moshi kama unapikia kuni…lakini mwenzetu Lowassa hakukubaliana na hayo, akaona kaonewa kwa madai anafaa kuwa rais mbona sisi tulikubali?," alihoji Sitta.
          
Aliendelea kusema, "hali hiyo, ilionesha ndani ya CCM kulikuwa na vyama viwili ambavyo ni 'CCM Katiba' na 'CCM Maslahi' ambayo alikuwa anaongoza Lowassa na mfuasi wake, Mgeja (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye pia alihamia Chadema hivi karibuni)."
          
Wanachama mapandikizi 
            Sitta alisema CCM ilikuwa              imejaa wanachama walio mapandikizi tofauti na sasa ambapo              alidai wamekwisha jionesha na kimekuwa chama kizuri kama              ilivyokuwa enzi za hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius              Nyerere.
          
Alisisitiza kwamba kitazidi              kuimarika na waliobaki wataendelea kutetea ilani na              kuhakikisha chama kinaendelea kushika dola. 
              
            Kwa mujibu wa Sitta, wakati wa              mchakato, baada ya kumaliza vikao, Lowassa alikuwa akiitisha              vikao vya kundi lake alilolibatiza CCM Maslahi na kuwaagiza              wapambe wake kuitisha vyombo vya habari kushambulia watu              ambao hawako kwenye mlengo wao.
          
Wakati huo huo mjumbe huyo wa NEC, alikumbusha umati uliohudhuria mkutano huo kwamba, uchaguzi wa mwaka huu unatumia Katiba ya zamani ya mwaka 1977 ambayo inatamka matokeo ya rais hayahojiwi hata kama aliyeshinda, amezidi kura moja.
          
Sitta ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, alisema alishauri wabunge wasitoke nje ya Bunge hilo waweze kutumia katiba hiyo iliyokuwa na kipengele cha kuhoji matokeo ya rais sasa imekula kwao.

0 comments:
Post a Comment