Hali ya              taharuki na wasiwasi mkubwa umewakumba wanafunzi wa shule ya              sekondari ya Selou katika wilaya ya Namtumbo mkoani              Ruvuma,baada ya wanafunzi wa kike kukumbwa na ugonjwa              usijulikana wa kutikisa vichwa bila kupumzika,kupiga kelele              na kukimbia kimbia ovyo.
                                                                
        Ndivyo ugonjwa huu wa                ajabu ulivyoibuka na kuwakumba wanafunzi wa kike katika                shule hii ya sekondari Selou-Namtumbo mkoani Ruvuma.
            Ni ugonjwa ambao                huwalazimu wanafunzi hawa kutikisa kichwa bila                kupumzika,kupiga kelele ambazo wakati mwingine ni kama                zinaashiria maumivu hivi.
            Na wakati mwingine                wakikosa uangalizi wa karibu hukimbia ovyo kusikojulikana.
            Wakati sintofahamu hii                ikileta shida na kuumiza vichwa vya walimu wa shule ya                Selou, wanafunzi wenyewe wanaeleza jinsi ugonjwa huo                unavyowaanza wenzao wakiwa darasani.
            Lakini mwalimu mkuu wa                shule ya sekondari ya Selou,Bwana Benny John anasema                tatizo hilo ambalo hutulia siku kadhaa na kuibuka tena                limedumu kwa takribani mwezi mmoja na tayari wataalamu wa                afya wa wilaya ya namtumbo walifika shuleni hapo kufanya                utabibu bila mafanikio. 
            Jitihada za kumpata                mganga mkuu wa wilaya ya Namtumbo kuzungumzia hali hii                zimegonga ukuta, lakini mkurugenzi wa halmashauri ya                wilaya hiyo,Bwana Ally Issa mpenyi anasema tatizo hilo                lilianza kwa watoto wawili na baadaye kuenea kwa wanafunzi                wengine na bado wanaendelea na uchunguzi.
          
0 comments:
Post a Comment