Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape              Nnauye.
        SASA ni dhahiri            kuwa mawaziri 11 wa Serikali ya Awamu ya Nne inayomaliza muda            wake, wametoswa katika mbio za kuwania ubunge kupitia Chama            Cha Mapinduzi (CCM), kati yao wakiwemo watatu ambao kura            katika majimbo yao zilirudiwa baada ya kulalamikiwa.
        Awali katika kura            za maoni za kupata wagombea ubunge wa CCM zilizofanyika nchi            nzima Agosti mosi mwaka huu, mawaziri tisa waliangushwa katika            kinyang'anyiro hicho, akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani ya            Nchi, Mathias Chikawe (Nachingwea) na Waziri wa Kazi na Ajira,            Gaundentia Kabaka (Tarime Mjini).
        Mbali na hao, pia            walikuwepo naibu mawaziri saba, akiwemo wa Mambo ya Nje na            Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, Pereira Ame            Silima (Mambo ya Ndani), Amos Makala (Maji), Kaika Saning'o            ole Telele (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi), Dk Makongoro            Mahanga (Kazi na Ajira), Adam Malima (Fedha) na Pindi Chana            (Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto).
        Baada ya kura hizo            za maoni, Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM iliyokaa wiki            hii, ilibaini kuwepo kwa kasoro katika kura za maoni            zilizofanyika katika majimbo 11 ambako zililalamikiwa,            yakiwemo matatu ya Busega mkoani Shinyanga, Rufiji mkoani            Pwani na Mahenge mkoani Iringa ambayo yalikuwa yakiwaniwa na            mawaziri watatu.
        Rufiji Katika Jimbo            la Rufiji wilayani Rufiji mkoani Pwani, Waziri wa Afya na            Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid, alijikuta akipata kura 5,010            na kuangushwa na Mohamed Mchengelwa, aliyejizolea kura 6,002.
        Katika kura za            maoni za awali, uchaguzi huo uliingia katika utata baada ya            kila upande kudai umeshinda, ambapo ilibidi uongozi wa CCM            Mkoa uingilie kati, lakini ufumbuzi haukupatikana hadi suala            hilo lilipopelekwa CCM Taifa na kuamuru uchaguzi huo ufanyike            tena ili kupata mshindi halali. Katika uchaguzi huo wa            marudio, jumla ya wagombea nane walijitokeza.
        Akitangaza matokeo            ya uchaguzi huo, ambao ulisimamiwa na kamati maalumu kutoka            CCM mkoa ili kuhakikisha uchaguzi huo unakwenda vizuri,            Msimamizi wa uchaguzi huo, Kombo Kamote ambaye pia ni Katibu            wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, alimtangaza mshindi huyo na kuamsha            shamrashamra kutoka kwa wapenzi wa Mchengelwa.
        Hata hivyo, wakati            matokeo hayo yakitangazwa Dk Seif hakuwepo ukumbini. Makete            Marudio ya kura katika Jimbo la Makete yaliyofanyika juzi,            yalishuhudia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais            (Mazingira), Dk Binilith Mahenge, akiangushwa na Mkuu wa            Wilaya ya Songea, Profesa Norman Sigalla.
        Akitangaza matokeo            hayo jana, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Mahenge, Jumanne Kapinga            alisema Profesa Sigalla alijizolea kura 8,883 na kufuatiwa na            Dk Mahenge aliyepata kura 7,885, Bonike Mhami (124), Fabian            Nkinga (74) na Lufunyo Nkinda (42).
        Awali katika kura            za maoni za mwanzo za Agosti Mosi mwaka huu, Dk Mahenge            aliongoza kupata kura 8,534 huku Profesa Sigalla akipata            8,211, Mhami (500), Nkingwa (486) na Nkinda (226).
        Kwa kile            kilichothibitisha kuwepo kwa udanganyifu wa matokeo ya awali,            baadhi ya wana CCM wa jimbo hilo walilazimika kusafiri hadi            makao makuu ya CCM ya wilaya ya Mahenge, kupinga matokeo hayo.
        Jery Slaa kidedea            Ukonga Mbali na mawaziri, katika Jimbo la Ukonga jijini Dar es            Salaam, ambako pia kura zilirudiwa, Meya wa Ilala, Jerry Silaa            ameshinda baada ya kupata kura 10,955, huku mfanyabiashara            maarufu, Ramesh Patel akishika nafasi ya pili kwa kupata kura            6,960.
        Silaa pia ni Mjumbe            wa Kamati Kuu ya CCM. Akitangaza matokeo hayo jana, Katibu            Msaidizi wa CCM Wilaya ya Ilala, Anastazia Mwonga alisema kwa            matokeo hayo, Slaa amepata ushindi wa asilimia 57.1 ya kura            zote, huku Patel akiambulia asilimia 36.3.
        Katika matokeo ya            awali, Silaa alishinda kwa kupata kura 10,000 huku Patel            akishika nafasi ya pili kwa kura 7,356. Namtumbo Vita 'chali'            tena Katika Jimbo la Namtumbo, kada wa chama hicho Edwin            Ngonyani, amembwaga tena mbunge aliyemaliza muda wake, Vita            Kawawa baada ya kupata kura 13,573 dhidi ya kura 10,068            alizopata Kawawa huku Balozi mstaafu wa Tanzania, Salome            Sijaona akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 6,015.
        Akitangaza matokeo            hayo, Mkurugenzi wa muda wa uchaguzi huo, Oscar Msigwa ambaye            ni Mjumbe wa NEC ya CCM Wilaya ya Njombe, alimtangaza Ngonyani            kuwa ndiye atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika            uchaguzi kwa kushindana na vyama vingine vya upinzani.
        
0 comments:
Post a Comment