August 15, 2015

  • PROFESA MSOLA ANGUKIAA PUA YA MAONI KILOLO



    PROFESA MSOLA ANGUKIAA PUA YA MAONI KILOLO

    NDOTO za Mshauri Mkuu wa Makamu wa Rais na mbunge wa Kilolo anayemaliza muda wake, Profesa Peter Msolla kuenelea kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo zimehitimishwa juzi katika kura za maoni za marudio zilizompa ushindi, Mkuu wa Wilaya wa Kaliua Tabora, Venance Mwamotto.
    Katika kinyanganyiro hicho, Profesa Msolla aliyewahi pia kuwa waziri wa wizara mbalimbali katika awamu ya kwanza ya serikali ya awamu ya nne alipata kura 9,810 dhidi ya kura 13,713 alizopata Mwamotto.
    Mbali na kuongoza wazira ya mawasiliano, sayansi na teknolojia, Profesa Msolla amewahi pia kuwa waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika.
    Na aliteuliwa kuwa Mshauri Mkuu wa Makamu wa Rais, Dk Gharib Mohamed Bilal baada ya kutemwa kwenye nafasi ya uwaziri katika awamu ya pili ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete.
    Kura hizo za maoni zilirudiwa katika jimbo hilo baada ya Kamati Kuu ya CCM kujiridhisha na malamamiko ya rafu na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi wa Agosti 1 yaliyotolewa na mbunge huyo.
    Katika uchaguzi huo wa awali, uliopelekea pia kata tatu kati ya 24 za jimbo hilo kurudia uchaguzi wake kwa kile kilichoelezwa kulikuwepo na udanganyifu katika mchakato wake wa upigaji kura, Mwamoto alishinda kwa kupata kura 11,200 huku Profesa Msolla akiwa mshindi wa pili kwa kujipatia kura 10,014.
    Kilonge
    Kabla kata hizo tatu za Lugalo, Uhambingeto na Nyarumbu hazijarudia uchaguzi huo ulioshirikisha wagombea 15, Profesa Msolla alikuwa akiongoza kwa kura 13,409 dhidi ya kura 9,749 alizopata Mwamotto.
    Kwa kupitia rufaa yake hiyo, Profesa Msolla alisema anapinga matokeo hayo kwasababu yalitangazwa bila kuridhiwa na wagombea au mawakala wao pamoja na kwamba alikuwa anaongoza kwa kura 13,409.
    Alisema kura zake ziliyoyoma baada ya Katibu wa wilaya bila kushirikisha kamati ya siasa ya wilaya hiyo kuamuru kata hizo kurudia uchaguzi kwa madai kwamba wasimamizi wa uchaguzi wa kata hizo walichelewa kuwasilisha matokeo yake ndani ya muda uliopangwa.
    "Na kimsingi kata zilizoamuriwa zirudie uchaguzi kwa kisingizio kwamba matokeo yake yalichelewa wakati kuna kata nyingine nyingi tu nazo zilichelewesha matokeo yake ni baadhi ya kata ambazo mimi nilipata kura nyingi zaidi ikilinganishwa na wagombea wengine," alisema.
    Alisema pamoja na kata hizo kuamriwa zirudie uchaguzi huo bila kufuata taratibu, vifaa vya kupigia kura vilifikishwa vituoni kwa kuchelewa na viliondolewa katika baadhi ya vituo hivyo kabla ya muda unaotakiwa.
    Alisema pamoja na kata hizo kurudia uchaguzi huo, uhesabuji wa matokeo ya jumla ya jimbo hilo uligubikwa na udanganyifu mkubwa kwani baadhi ya vituo alivyoongoza kwa kura; kura hizo hazikuwepo tena.
    Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo majuzi usiku , Katibu wa CCM wa wilaya ya Kilolo aliwataja wagombea wengine na kura zao kwenye mabano kuwa ni Danford Mbilinyi (1,142), Chelestino Mofuga (576), Merick Luvinga (161), Thadei Kikoti (136), Yefred Myenzi (63) na Anosta Nyamoga (68).
    Wengine ni Luciana Mwambosa (53), Mgabe Kihongosi (46), Francis Mkokwa (47), Ashraf Chusi (29), Abdul Mkakatu (28), Basike Mteleka (17) na Israel Sarufu (9).- See more at: http://mtovisala.blogspot.com/2015/08/prof-msolla-abwagwahoi-tena-kura-za.html#sthash.bGx7J3ia.dpuf


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.