August 25, 2015

  • Aliyewahi Kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha Ambaye Kwa Sasa ni Mwanachama wa CHADEMA Akamatwa na Jeshi la Polisi



    Aliyewahi Kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha Ambaye Kwa Sasa ni Mwanachama wa CHADEMA Akamatwa na Jeshi la Polisi
    Aliyekuwa waziri wa Mashauri ya Ndani ambae sasa ni mwanachama wa CHADEMA Mh Laurance Masha amekamatwa jioni ya leo na jeshi la polisi nchini.

    Tukio la kukamatwa Masha limefuatia kukamatwa kwa wanachama 18 waliokuwa kwenye harakati za kawaida za uenezi wa chama chao katika kampeni ya kawaida ya nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu ambayo haizuiwi na sheria yoyote ile nchini.

    Baada ya kukamatwa vijana hao na kufikishwa kituo cha Ostarbay, Mh Masha aliamua kwenda kufuatilia sababu za kukamatwa kwa wanaukombozi hao, ajabu alipofika tu nae akatiwa mbaroni.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.