Chama                Cha Mapinduzi (CCM).
            Ameihama                  CCM kwa kile alichodai kufanyiwa mizengwe ya mara kwa                  mara na viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya.
          Kada wa Chama Cha Mapinduzi                  (CCM) aliyeshindwa kura za maoni za ubunge katika Jimbo                  la Bunda,  mkoani Mara, Maximillian Madoro, amejiondoa                  kwenye chama hicho na kuomba uanachama wa chama cha                  Democratic Party (DP) ili awanie ubunge jimbo hilo.
              Awali Madoro alikuwa Diwani wa                  CCM kata ya Nyamuswa, wilayani Bunda. 
              Akizungumza na waandishi wa                  habari mjini hapa jana, Madoro alisema ameihama CCM kwa                  kile alichodai kufanyiwa mizengwe ya mara kwa mara na                  viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya.
              Alidai katika uchaguzi huo wa                  kura za maoni aliwekewa mizengwe ya kila aina na                  viongozi wa CCM ngazi ya wilaya, ikiwamo kumtangaza                  ameshika nafasi ya tatu kwa kupata kura 1,935 katika                  kinyang'anyiro hicho wakati alikuwa mshindi wa pili kwa                  madai ya kupata kura 2,276.
              Akieleza kilichomsukuma                  kugombea ubunge katika jimbo hilo kupitia DP, Madoro                  alisema lengo ni kutaka kuwaletea maendeleo wananchi wa                  jimbo hilo katika sekta ya elimu, maji, afya na                  miundombinu.
              Mwenyekiti wa CCM Wilayani                  Bunda, Chacha Gimanwa, alithibitisha kada huyo kukihama                  chama hicho na kukanusha kufanyiwa mizengwe, akisema                  amehama kwa utashi wake baada ya kukosa nafasi ya                  kuwania ubunge kupitia chama hicho.
            
0 comments:
Post a Comment