Idadi                    ya wanafunzi  wanaopata  mikopo kutoka   Bodi ya                    Mikopo  kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imekuwa                    imeongezeka mwaka hadi mwaka na kusaidia kuongeza                    idadi ya watanzania wanaopata elimu ya juu.
          Katika                    mwaka wa masomo wa 2005/2006 Bodi ya Mikopo ilitoa                    mikopo kwa  wanafunzi 42,729 iliyogharimu sh.  bilioni                    56.1  na mwaka wa masomo wa 2014/2015 bodi ya mikopo                    ilitoa mikopo kwa wanafunzi 98,000 iliyogharimu                    shilingi bilioni 345.
          Hayo                    yalisemawa leo na Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi wa                    Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka bodi hiyo Cosmas                    Mwaisobwa wakati akizungumza na waandishi wa  habari                    kwenye ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (MAELEZO)                    kuhusu mafanikio ya  bodi hiyo katika kipindi hicho.
          Alisema                    kwa kipindi hicho chote  wamekuwa na sheria mbalimbali                    ilioanzishwa kwa kuwapa jukumu la ukusanyaji wa madeni                    ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ambayo ilianza                    kutolewa tangu mwaka 1994/1995 kupitia iliyokuwa                    Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia wakati huo                    Serikali haikukusanya madeni kutoka kwa wanufaika hadi                    pale bodi  ilipoanza kazi rasmi mwaka 2006/2007.
          Aliongeza                    kuwa taasisi hiyo imekuwa  na mafanikio makubwa                    kulinganisha na hapo awali kwani kwa kipindi cha miaka                    kumi tumeongeza ufanisi katika matumizi ya                    teknolojia  ya habari na mawasiliano (TEHAMA)  kwa                    lengo la kuomba mikopo kwa njia ya mtandao kupitia                    mfumo wa uombaji wa mikopo  wa (OLAMS)
          Aidha  bodi                    hiyo  imeendelea kukua kwa kasi kutokana na idadi ya                    watumishi kutoka tisa hadi kufikia watumishi 135 mwaka                    huu,ongezeko hilo limesaidia bodi kuwa na ufanisi                    katika utekelezaji wa majukumu yake.
          Bodi                    hiyo imewawezesha wateja wake  kupata huduma katika                    maeneo manne ambayo ni  Arusha, Mwanza, Dodoma, na                    Zanzibar ili kupata huduma za kibodi kwa ukaribu                    zaidi.
          Mwaisongwa   aliwahakikishia                    wateja  hao  wataendelea kuwanufaisha waombaji na                    kutambua kuwa mikopo ya wanafunzi  wa elimu ya  juu ni                    sehemu ya utekelezaji wa sera ya uchangiaji wa elimu                    ya juu na ni muhimu kurejesha mikopo ili kuwezesha                    mfuko huo  kuwa endelevu.
          Taasisi                    hiyo iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria namba  9 ya                    mwaka 2004 na kuanza rasmi julai 2005 yenye lengo la                    kutoa mikopo kwa wanafunzi i wa elimu ya juu,utoaji na                    ukusanyaji wa mikopo ili kufanya mfuko wa mikopo kuwa                    endelevu.
          
0 comments:
Post a Comment