Wanachama          kumi wa kundi la Boko Haram, wameuawa kwa kupigwa risasi nchini          Chad.
        Wapiganaji          hao walipewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya          kuhusika na vitendo vya kigaidi, katika kesi iliyofanyika katika          mji mkuu wa nchi hiyo N'Djamena.
        Maafisa          wa ulinzi wanasema kwamba waasi hao waliuawa na kitengo maalum          cha ulinzi Kaskazini mwa mji mkuu.
        Washukiwa          hao kumi walihukumiwa kuhusiana na mashambulio mawili          yaliyotokea katika mji mkuu mwezi Juni, mwaka huu, mashambulio          yaliyosababisha vifo vya watu 38.
        Lakini          mwezi mmoja baada ya shambulio hilo, serikali ya Chad ilirejesha          tena adhabu ya kifo, kwa washukiwa wanaopatikana na hatia ya          ugaidi.
        Miongoni          mwa waliouawa ni Mohamat Mustapha, anayejulikana kwa jina          lingine kama Bana Fanaye, ambaye ametajwa kama kiongozi wa          mashambulio ya Juni.
        Shule          moja ya umma na kituo cha polisi kililengwa na walipuaji wa          kujitolea waliokuwa kwenye piki piki, na kuwaacha zaidi ya watu          mia moja na majeraha, mbali na waliouawa.
        Baada          ya mashambulio hayo ya Juni, soko moja maarufu katika mji mkuu          ulishambuliwa na watu kumi na watano kuuawa.
        Mashumbulizi          hayo yalikuwa ya kwanza kuwahi kutekelezwa na wapiganaji hao          kutoka Nigeria, nchini Chad ambayo inawahifadhi wanajeshi wa          muungano ambao wanaendeleza harakati za kupambana na kundi hilo.
        Kwa          mujibu wa mwendesha mashtaka mkuu, Bruno Mahouli Louapambe,          washukiwa hao walipatikana na hatia ya mashtaka kadhaa yakiwemo,          njama ya kutekeleza uhalifu, mauaji, kuharibu mali kimakusudi          wakitumia vilipuzi, ulaghai, kumiliki silaha na risasi bila          idhini na kutumia bidhaa ambazo zinaweza kusababisha maangamizi.
        Chad          imekuwa katika mstari wa mbele kuisaidi Nigeria, kuyakomboa          maeneo yaliyotekwa na wapiganaji hao wa Boko Haram.
        Wanamgambo          hao wa Kiislamu, ambao wanataka kuunda Jamuhuri yao ya Kiislamu          nchini Nigeria, wamewauawa maelfu ya raia na kuwalazimisha          mamilioni ya wengine kukimbia makwao Kaskazini Mashariki mwa          nchi hiyo tangu 2009.
        Kundi          hilo lilikuwa limetishia kushambulia Chad, baada ya serikali ya          nchi hiyo kutuma wanajeshi wake nchini Nigeria, kupambana na          kundi hilo na kukomboa maeneo waliyoyateka hasa katika jimbo la          Borno.
        Kufuatia          mashambulio hayo ya ,Chad ilipiga Marufu watu wote nchini humo          kuvalia vitambaaa vinavyofunika nyuso zao, maarufu kama Burka.
        Lakini          juhudi ya kudhibiti kundi hilo na ugaidi zimeshutumiwa na          upinzani na makundi ya kutetea haki za kibinadam ambao wana wasi          wasi kuwa huenda serikali ikahujumu haki za raia, kwa misingi ya          kupambana na ugaidi.
        Wasifu wa Boko Haram
- Boko Haram lilianzishwa mwaka wa 2002, dhamira kuu ikiwa kupinga mfumo wa elimu kutoka mataifa ya Magharibi. Boko Haram linamaanisha Elimu kutoka mataifa ya Magharibi imepigwa marufuku, kwa lugha ya Kihausa.
 - Kundi hilo lilianzisha operesheni za kijeshi 2009.
 - Maelfu ya watu wameuawa, wengi wao kutoka eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, wamewateka nyara mamia ya wengine wakiwemo wasichana 200 wa shule ya wasichana ya Chibok.
 - Iliijiunga na kundi la Islamic State na sasa limegeuza jina lake na kuwa Islamic State iliyo Magharibi wa Afrika au"West African province".
 - Boko Haram limeteka eneo kubwa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, ambako limetangaza kuwa ni taifa huru la Kiislamu.
 - Wanajeshi wa Muungano hata hivyo wamefanikiwa kuyakomboa baadhi ya maeneo hayo.
 - BBC.
 
0 comments:
Post a Comment