Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limemkamata na kumfikisha mahakamani Daktari Feki Halima Sanga kwa kosa la kugushi vyeti vya udaktari daraja la pili na kisha kupangiwa kazi na wizara ya afya na ustawi wa jamii Hospitali ya mkoa wa Ligula.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Henrry Mwaibambe amesema taarifa za mtuhumiwa huyo ziliwafikia baada ya madaktari wa hospitali ya Ligula kubaini mtuhumiwa huyo hafahamu mambo ya msingi ya udaktari.
Amesema mtuhumiwa ambaye jina lake halali ni Halima Sanga, amekuwa akitumia jina la Dr.Sara Matuja na aliajiriwa na wizara ya afya 26-5-2015 na kufanya mazoezi ya udaktari katika hospitali ya rufaa ya muhimbili kabla ya kupangiwa kazi hospitali ya mkoa wa Ligula.
Hata hivyo kamanda Mwaibambe amesema baada ya Dokta.Sara Matuja ambaye yuko hospitali ya rufaa ya Bugando, kupigiwa simu alikiri ni vyeti vyake na kudai huwenda mtuhumiwa alivipata maeneo ambayo alivisambaza kuomba ajira,huku akisisitiza uchunguzi unafanyika ili kubaini alipataje kazi serikalini.
Kamanda amekiri binti huyo mwenye umri wa miaka 27 ni hatari kutokana na matukio ya nyuma ambapo gazeti la uwazi mwaka 2013 liliwahi kumkariri akisema aliyekuwa wazirimwanamke huyo ni mtu hatari.
ITV
0 comments:
Post a Comment