August 19, 2015

  • BIASHARA YA DHAHABU KUBORESHWA TANZANIA


    BIASHARA YA DHAHABU KUBORESHWA TANZANIA
    Kwa watu wengi, pete ya dhahabu ni ishara ya upendo wa milele, lakini mara nyingine simulizi nyuma ya dhahabu hiyo huwa si ya kufurahisha sana.


    Tanzania ni mzalishaji wanne wa dhahabu barani Afrika - lakini mamia ya maelfu ya wachimbaji wadogo wadogo nchini humo hufanya kazi katika mazingira magumu sana huku wakipata ujira mdogo na hata kuwa na matumaini madogo ya mafanikio yao.
    Lakini inawezekana hili likabadilika kufuatia mpango mpya ulioandaliwa na shirika la Fairtrade kuuza dhahabu hiyo Uingereza - mpango huu ni wa kwanza wa aina yake barani Afrika.
    Haya ndio mazingira waliyonayo wachimbaji wadogo wadogo wengi nchini Tanzania
    Lakini kilomita moja kutoka hapa ni mgodi wa Nsagano.
    Mgodi huu unatarajiwa kuwa mgodi wa kwanza Tanzania kuuza dhahabu Uingereza chini ya mkataba wa fairtrade.
    Mkataba huo unahakiksha ufuatialiaji wa vigezo vya afya na usalama katika mgodi pamoja na malipo bora Zaidi.
    Akiinama mbele ya beseni la blue ikiwa na maji yenye rangi la tope, Prisca Alexi anavuruga matope ya malighafi ya dhahabu pamoja na zebaki.
    Huku akiwa amevaa glavui nyukundu mikononi mwake, anafanyakazi yake ya kucheka mchanga huo na karai, akiwa makini maji hayo yasiguse ngozi yake.
    Prisca anafanya kazi kama mchekechaji, lakini anasema ujira anaoupata ni mdogo mno.
    Mazingira ya hapa ni duni sana, mbali na wachimbaji kuvaa fulana za kazi, kofia ngumu na glavu.
    Alan Frampton ni mkurugenzi wa Cred jewellery inayoiagiza dhahabu ya fairtrade nchini Uingereza.
    Anasema kuna uhitaji mkubwa kutoka kwa wateja kufahamu mazingira ambayo bidhaa inatoka
    Lakini mchambuzi wa maswala ya uchumi anasema aina ya mipango hii inaweza kuharibu utaratibu wa kiuchumi wa biashara za ndani.
    Dr Donald Mmari ni mkurugenzi wa utafiti na maendeleo katika shirika la utafiti, REPOA
    'Huu ni mpango pekee ambao unatarajiwa kunufaisha wachimbaji zaidi ya 200 katika mgodi mmoja, wakati ambapo wengi wao wengine wataendelea kusota kwa maisha ambayo hayafanani kabisa na wanachokichimba'.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.