August 25, 2015

  • 'HAPA NI NYUMBANI KWANGU': KARIM BENZEMA APUUZA UVUMI WA KUSAJILIWA ARSENAL


    'HAPA NI NYUMBANI KWANGU': KARIM BENZEMA APUUZA UVUMI WA KUSAJILIWA ARSENAL
    Karim Benzema amezipuuza habari zinazodai kuwa anaweza akaondoka Real Madrid kabla dirisha la usajili halijafungwa.
    Kwa miezi ya hivi karibuni, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa akihusishwa na usajili wa kwenda Arsenal huku ripoti zilizotoka wikiendi zikidai alipaa kwenda London kujadili uhamisho huo.
    Benzema amefanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Real Madrid Jumatatu katika maandalizi ya mechi ijayo ya La Liga baada ya kuwa na mwanzo mbovu Jumapili kwa sare tasa dhidi ya Sporting Gijon.
    Katika kuwakata maini wanaodhani kuwa anaondoka, Benzema akatupia picha kwenye ukurasa wake wa Twitter na kusema Real Madrid ni nyumbani kwake na ana furaha kuwa hapo.





  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.