Halmashauri ya wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro imeanza kuchukua hatua za kukagua madaftari yote yaliyokuwa na majina ya wapiga kura na kubaini majina ya wanachi 1750 waliojiandisha na kuapata shahada za kupiga kura majina yao hayaonekani.
Msimazi mkuu wa uchaguzi katika jimbo la siha Bw.Rashid Kitambulio ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuhusiana na changamoto ambazo zimejitokeza wakati wa kuhakiki majina ya wananchi waliojiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura mwaka huu.
Amesema tayari wameshawasiliana tume ya taifa ya uchaguzi makao maku jijini Dar es Salaam kuhusu kasoro na mapungufu yaliyojitokeza ya kukosekana kwa baadhi ya majina ya wapiga kura wenye shahada kwa baadhi ya vituo na kwamba tatizo hilo linashughulikiwa mapema ili kuhakikisha majina yaliyokosekana yanarejeshwa mapema iwezekanavyo.
Naye mratibu wa uchaguzi wilaya siha Bw.Stanley Coola amesema kasoro zilizojitokeza zitafanyiwa marekebisho kabla ya kupiga kura na kwamba zoezi nhilo la uhakiki linaendelea ili kuwezesha wananchi waliojiandikisha kuweza kupata nhaki yao ya msingi ya kupiga kura ifikapo oktoba 25 mwaka huu.
Katika jimbo la Siha jumla ya wananchi 55,011 wameandikishwa na kwamba lengo lilikuwa ni kuandisha wananchi 65,038 hali ambayo amewataka wananchi waliojiandisha kujitokeza katika vituo vya uhakiki wa majina yao katika daftari la kudumu la kupiga kura.
0 comments:
Post a Comment