August 15, 2015

  • MBARAWA ATOA ELIMU YA SHERIA YA MITANDAO



    MBARAWA ATOA ELIMU YA SHERIA YA MITANDAO
    Serikali imesema Shilingi Trilioni 54.4 zitakuwa kwenye hatari ya kuingia katika mikono ya wahalifu wa mitandao, endapo Sheria za Usalama wa Mitandao na Miamala ya fedha haitatumika.


     
    Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa (pichani), wakati akifungua mafunzo ya viongozi wa Jeshi la Polisi iliyolenga kuwapa elimu kuhusu utekelezaji wa sheria hizo kabla ya kuanza kutumika Septemba mosi, mwaka huu.
     
    Alisema fedha hizo sawa na Trioni 4.4 kila mwezi, watu wanahifadhi na kutuma kupitia miamala mbalimbali ya mitandao ya simu za mikononi.
     
    Profesa Mbarawa, alisema fedha hizo lazima zilindwe kwa kuwekewa sheria zenye kuzuia na kutoa adhabu kali kwa watu watakaoingilia mihamala ya kifedha.  
     
    Sheria hizo ambazo Rais Jakaya Kikwete ameridhia kwa kutia saini hivi karibuni, zimelalamikiwa na Wananchi wa kada mbali mbali kutokana na kuwa na vipengele vinavyokandamiza haki ya kutafuta na kupata habari.
    "Sheria hizi zilikuwa zikilalamikiwa na baadhi ya watu kwamba zinakiuka haki za binadamu, lakini ukweli lengo lake ni kuilinda nchi dhidi ya wahalifu na hasa usalama wa nchi na miamala ya kifedha inayofanyika kila siku," alisema. Hata hivyo, aliwataka wadau wanaoweza kufanya uchambuzi  kwa ajili ya kurekebisha sheria hizo wapo tayari kupokea na kufanyia kazi.
     
    Aidha, Profesa Mbarawa alieleza sheria hizo zinazoweza kubadilika kwa kufanyiwa marekebisho kulingana na mahitaji ya watu, yeye kama Waziri yupo tayari kupokea ushauri huo kwa manufaa ya nchi.'Sisi siyo nchi ya kwanza kutunga sheria kama hizi, zipo nyingi tu, hatuwezi kuepuka hata mara moja, Nafikiri jambo la  muhimu hapa ni kuweka ushirikiano kati ya serikali na wadau katika kuboresha sheria hizi, tupo tayari kupokea na kufanyia kazi," alisisitiza. Alisema lengo la Wizara yake kuanza na jeshi hilo katika mpango wake wa utoaji wa elimu ni kuhakikisha sheria hizo zinafahamika na kueleweka na askari ambao kazi yao ni kuwazuia watu wasivunje sheria.
     
    Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, Kamishna wa Polisi, Musa Ali Musa, alisema watatumia mafunzo hayo kama njia ya kulitengeneza jeshi hilo kukabiliana na matukio ya wizi unaotumia teknolojia ya kimtandao

    NIPASHE


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.