August 26, 2015

  • Afariki kwa kufukiwa na kifusi akichimba Madini.



    Afariki kwa kufukiwa na kifusi akichimba Madini.
    Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Kutiba Amani mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa kijiji cha Luegu wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,amekutwa akiwa amefariki Dunia na mwili wake kuharibika vibaya mara baada kufukiwa na kifusi akichimba madini aina ya Quamalin katika machimbo ya Mtwara.




    Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma,Bw.Mihayo Msikhela amesema mtu huyo aliondoka nyumbani kwake wiki mbili zilizopita kwenda katika machimbo hayo ya kijiji cha mtwara Wilaya ya Namtumbo kwa lengo la kuchimba madini aina ya Quamalin yanayo patikana katika machimbo hayo lakini siku chache zilizopita eneo hilo lilianza kutawaliwa na harufu kali ikitokea kwenye moja ya shimo alimokua akichimba.
     
    Hata hivyo siku mbili baadaye hofu ya wananchi kwamba kulikua na mwili zaidi ya mmoja ilianza kutanda zaidi kutokana na harufu kuendelea kuwa kali,na ndipo kamanda Msikhela akiongozana na daktari wa wilaya ya namtumbo na maafisa wa madini mkoa wa Ruvuma kuendesha upya zoezi la ufukuaji na kufanikiwa kupata mabaki ya eneo la mdomo wa chini ya mwili wa awali na kwamba hakuna miili mingine.
     
    Uchimbaji wa madini hayo kwa staili ya "FONKA" unaofanywa na wachimbaji wadogo katika maeneo mengi hapa mkoani ruvuma ni moja ya uchimbaji hatari ambapo wizara inayoshughulikia masuala ya madini imepiga marufuku.

    CHANZO:ITV.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.