Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec),            imetangaza siku ya urejeshaji fomu za Urais na Makamu wa rais            kuwa ni Alhamis ijayo.
        Aidha, imepiga marufuku maandamano            na badala yake watu saba tu ndio wataruhusiwa kusindikiza            wagombea.
        Taarifa ya Nec kwa vyombo vya habari            jana na kusainiwa na Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima,            ilisema urejeshaji fomu utaanza saa 1:30 asubuhi hadi saa            10:00 jioni.
        Alisema wagombea wote wanatakiwa            kufika kwenye ofisi za Tume wakisindikizwa na watu hao na            majina yao yawasilishwe Tume kabla ya Agosti 20, ili kuratibu            kazi hiyo.
        "Wagombea hawaruhusiwi kuja Tume kwa            maandamano, shamrashamra, nderemo wala vifijo. Hii ni kwa            sababu siku hiyo vyama vya siasa vitakavyowasilisha fomu za            kuomba uteuzi vitakuwa vingi hivyo kila chama kikija Tume kwa            maandamano na shamrashamra kunaweza kutokea uvujifu wa amani,"            alisema.
        Alisema sababu nyingine ni            kuwawezesha wananchi wengine kuendelea na shughuli zao na            sababu ya tatu ni kuimarisha amani na utulivu na kwamba ni            vyem vyama vikafuata maelekezo hayo
        
0 comments:
Post a Comment