Chama cha Wananchi (CUF) kimetangaza wagombea wa nafasi ya ubunge na uwakilishi kwa majimbo 54 ya uchaguzi kwa nafasi na uwakilishi na majimbo 50 kwa nafasi ya ubunge huku kikimtema kigogo wake, Muhammed Habibu Mnyaa (pichani), baada ya jimbo lake la Mkanyageni kufutwa na Tume ya Uchaguzi (Zec).
Mkurugenzi wa uchaguzi wa chama            hicho, Omar Ali Shehe, alisema baada ya Zec kufanya mabadiliko            ya mgawanyo wa majimbo na kuongeza majimbo manne mapya, chama            hicho kililazimika kufanya mabadiliko ya wagombea wa majimbo.
          
          
        Alisema baadhi ya wagombea            waliogombea majimbo ya zamani na sasa yamebadilishwa majina            wamewapa majimbo hayo yaliobadilishwa majina na kuwaongeza            wagombea wanne kwa majimbo mapya kwa nafasi za uwakilishi.
          
          
        Mnyaa alikataliwa na wananchi katika            kura za maoni, lakini baadaye Baraza Kuu la Uongozi            likapitisha jina lake kugombea nafasi hiyo, hatua iliyoibua            malalamiko kutoka kwa wanachama wa CUF kwa madai ya kuwa            hakuwa chaguo lao.
          
          
        Baraza Kuu la CUF lilirejesha jina            la Mnyaa kabla ya Zec kutoa ripoti ya mapitio na mgawanyo wa            majimbo na baada ya kumaliza kazi hiyo tume ililifuta jimbo la            Mkanyageni alilokuwa akiliongoza.
          
          
        Shehe alisema jana kuwa utaratibu            uliotumika katika kuwapata wagombea wa majimbo mapya wamefuata            katiba ya chama ambayo inaruhusu kufanya mabadiliko katika            hali ya dharura.
          
          
        Aidha, CUF imemrejesha Naibu Naziri            wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati, Haji Makame Mwadini ambaye            alibwagwa katika kura za maoni kutetea nafasi yake  ya            uwakilishi kwa jimbo la Nungwi na jina lake halikurejeshwa na            Baraza Kuu la chama hicho, lakini sasa amepewa kugombea jimbo            la Kijini.
          
          
        Waliobadilishwa majimbo baada ya            Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kutaja majina mapya kwa baadhi            ya majimbo ni Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu (sasa Malindi)            wakati ni Ali Saleh aliyekuwa anagombea ubunge Mji Mkongwe            (sasa Malindi).
          
          
        Wengine ni mwakilishi wa jimbo la            Mtoni, Nassor Ahmed Mazrui amepelekwa  jimbo la Mtopepo,            Mansour Yussuf Himid uwakilishi jimbo la Chukwani badala ya            Kiembe Samaki na Abdillahi Jihadi Hassan uwakilishi jimbo la            Mwanakwerekwe badala ya Magogoni
        
0 comments:
Post a Comment