Mgombea Ubunge katika Jimbo la Ludewa kwa tiketi ya CCM Bw. Deo Filikunjombe, amepita bila kupingwa wilayani humo baada ya Mgombea wa Chadema kushindwa kutimiza Masharti na Taratibu za Ujazaji wa Fomu.
Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya              Ludewa, Ndg. Wiliam Waziri amesema leo kuwa Mgombea wa              Chadema ameshindwa kutimiza taratibu za ujazaji wa fomu hizo              hivyo kukosa sifa ya kuwa Mgombea wa Ubunge.
        Ndg. Waziri amesema kwamba Kati              ya wagombea wanne waliochukua fomu aliyetimiza taratibu ni              Mgombea wa CCM, Bw. Deo Filikunjombe pekee;
        Wagombea wa DP na TLP              waliishindwa kabisa kurejesha fomu huku Mgombea wa Chadema              akishindwa kujaza fomu vizuri na kushindwa kurejesha Fomu ya              Kiapo cha Maadili ya Sheria za Uchaguzi.
        
0 comments:
Post a Comment