Mgombea Urais wa tiketi ya UKAWA, Edward Lowassa            akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Tandale. Kushoto            kwake ni Mgombea Mwenza, Juma Duni HajiJESHI la              Polisi Dar es Salaam leo limevamia na kuuzuia msafara wa              mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo              (Chadema), Edward Lowassa kuingia sokoni Kariakoo.
        Polisi hao              walikuwa kwenye magari aina ya Land Rover huku wakiwa na              silaha za moto tayari kukabiliana na hali yoyote, walimzuia              Lowassa ambaye alikusudia kwenda Kariakoo shimoni.
        Lowassa alifika                Mtaa wa Swahili saa 6:09 mchana ikiwa ni mtaa mmoja kabla                ya kuingia sokoni shimoni ambapo alikusudia kusalimia                wafanyabiashara hao kama alivyofanya Tandale na Tandika.
            Kabla ya kufika                Mtaa wa Swahili, msafara wa Lowassa ulianzia katika Soko                la Tandale na baadaye alikwenda Tandika kusalimia                wafanyabiashara na wakazi wa maeneo hayo.
            Polisi                walimvamia na kuamuru msafara wake kuishia Mtaa wa Swahili                kwa kile walichoeleza kutokuwepo kwa taarifa ya ujio wake                pamoja na kuepusha msongamano ambao tayari ulianza                kutokea.
            Msafara wa                Lowassa ulisindikizwa na wafanyabiashara wa Kariakoo                waliojitokeza kumpoke huku wakiimba nyimbo za kumsifu,                ambao pia walinyimwa fursa ya kumuona.
            Waliimba "si si                si… si mnaona, mziki wa Lowassa kuutuliza hamuwezi,"                maneno waliyoyarudia mara kwa mara.
            Polisi                wamesema, Lowassa ambaye alikuwa ameongozana na kundi                kubwa la vijana hakutoa taarifa mapema ili waimarishe                ulinzi. Hata hivyo kulikuwa na majadiliano kati ya Kamanda                wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Lucas Mkondya na maofisa                wa Chadema.
            Makubaliano                yalihitimishwa kwa Lowassa na maofisa wake kukubali                kutofika sokoni mahala alipotarajia kukutana na kuzungumza                na wafanyabiashara hao.
            Alipokuwa Tandale
            Lowassa alitoka                nyumbani nyumbani kwake Masaki saa 2:35 asubui na kuelekea                katika Soko la Tandale.
            Kabla ya kufika                sokoni Tandale, wananchi waliomwona kwenye gari walianza                kumfuata, hata hivyo alikwenda mpaka sokoni ambapo alifika                saa 3:20 ambapo alizungumza na wafanyabiashara wa hapo.
            Said Omary                ambaye ni mfanyabiashara wa nafaka alimwomba Lowassa kuwa,                akifanikiwa kutwaa nchi awaboreshee miundombinu ya                barabara ili kurahisisha kuingiza bidhaa zao.
            "Soko halina                ubora wowote maana CCM wanachangisha ushuru lakini                hawalihudumii. Ni bora tuachiwe wenyewe tuliendeshe maana                tunalipa ushuru wa bure."
            Omary alisema                hayo baada ya kuulizwa na Lowassa kwamba, endapo ataingia                madarakan, angependa amfanyie nini?
            Kabla ya                kuondoka Lowassa alinunua maharage kwa Sh. 30,000 kutoka                kwa mfanyabiashara huyo. Baadaye alikwenda kwa                mfanyabiashara wa miwa aliyejitambulisha kwa jina la                Gerard.
            Gerard                amemwambia Lowassa "tunaomba ukiingia madarakani                utukumbuke sisi vijana wako kwa kutupatia ajira ya kutosha                maana hii biashara haina faida." Alipofika kwa muuza                maziwa Lowassa alinunua kikombe kimoja na kunywa fundo                moja.
            Alimaliza                sokoni hapo saa 3:50 gari lake likisindikizwa na mamia ya                watu pia akisindikizwa na vijana wa bodaboda.
            Kwenda Tandika
            Msafara                uliingia katika Barabara ya Morogoro saa 4:01 asubuhi na                kufuatiwa na pikipiki huku zikiwa zimebeba watu ambao                walikuwa wakiimba nyimbo za kumsifu.
            Msafara                uliingia Barabara ya Mandela na kukuta wananchi wakiwa                wamejipanga kumsalimia kwa kumpungia mikono huku na yeye                akifanya hivyo.
            Alifika Soko la                Tandika saa 4:33 asubuhi ambapo shughuli zilisimama kwa                muda huku mamia ya watu waliojaa sokoni hapo wakitaka                kumuona.
            Lowassa bila ya                kujali hali ya soko kuwa chafu, aliingia ndani na                kuangalia bidhaa mbalimbali na bei zake.
            Lowassa akiwa                ndani ya soko hilo alipata fursa ya kuzungumza na muuza                maji ya kufunga maarufu kama 'kandoro' ambaye hakutaja                jina lake.
            Alimuuliza                kijana huyo kiasi gani anapata kutokana na biashara hiyo?                alimjibu "hakuna faida yoyote, tunaganga njaa tu ilimradi                mkono uende kinywani."
            Aidha, wananchi                wengine waliokuwa wamefurika sokoni hapo walisikika                wakisema "Baba tunakuomba uingiapo madarakani, utujengee                soko letu maana halina hadhi, ni chafu na linanuka. CCM                wameshindwa kazi, wanakula pesa zetu tu."
            Hata hivyo,                wananchi wengi wa sokoni hapo walipoulizwa ni kwanini                wameacha shughuli zao na kumsikiliza Lowassa, wamejibu                "huyo ndio rais tunayemuhitaji ambaye akiwa madarakani                atajua aanzie wapi kutatua shida zetu. Rais anatakiwa kuwa                mtu wa watu kama huyu, hapa kashapita."
          
0 comments:
Post a Comment