Rais          wa Burundi Pierre Nkurunziza anaapishwa kwa muhula wa tatu          uliozua utata.
        Mwandishi          wa BBC Prime Ndikumagenge nchini Burundi anasema kuwa sherehe          hiyo imefanyika kwa mshangao mkubwa kwa kuwa rais Nkurunziza          alitarajiwa kuapishwa wiki ijayo.
        Hatahivyo          hakuna kiongozi wa taifa lolote aliyehudhuria sherehe za          kuapishwa kwake huku Afrika kusini ikishirikishwa na waziri          mmoja kulingana na shirika AFP.
        Mataifa          kadhaa yakiwemo yale ya China na Urusi yalituma mabalozi wao.
        Mabalozi          wa Marekani na muungano wa Ulaya walisusia lakini          wakashirikishwa na maafisa wa nyadhfa za chini.
        Umoja          wa Afrika haukutuma waangalizi.
        Takriban          watu 10 wameuawa tangu Nkurunziza atangaze mnamo mwezi Aprili          kwamba atawania muhula wa tatu wa urais.
        Serikali          inaushtumu upinzani ambao unasema kuwa muhula huo ni kinyume na          sheria kwa kuzua ghasia.
        Umoja          wa Afrika,muungano wa Ulaya na wizara ya maswala ya kigeni ya          Marekani wote wameonyesha wasiwasi wao kwamba uchaguzi huo wa          mwezi Julai haukuwa huru na wa haki.
        BBC
        
0 comments:
Post a Comment