August 25, 2015

  • VIFAA VYA HALI YA HEWA TATIZO AFRIKA


    VIFAA VYA HALI YA HEWA TATIZO AFRIKA

    Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba 
    Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi amesema nchi za Afrika zina upungufu wa vifaa vya kutambua mvua zitakazonyesha kama ni El Nino.


    Kijazi alisema hayo jana alipokutana na wataalamu wa mamlaka ya hali ya hewa kutoka nchi za Afrika waliokutana kujadili na kuchukua hatua ya kukabiliana na majanga yatakayoambatana na mvua hizo.
    Dk Kijazi alisema wataalamu hao wanashindwa kuendesha kwa ufanisi shughuli za utabiri kutokana na vifaa kushindwa kutambua athari za mvua zitakazonyesha.
    "Tumekutana nchi 11 za Afrika ili kila nchi iweze kuchukua tahadhari ya mvua za El Nino... na tunasisitiza Serikali za nchi husika ziongeze vifaa vya kutosha vya kupima na kuchambua taarifa za hali ya hewa ili utabiri uwe wa ufanisi," alisema Dk Kijazi.
    Alisema hadi jana kipimo cha utabiri wa hali ya hewa kilikuwa kinaonyesha joto halijaongezeka katika Bahari ya Hindi, endapo kutakuwa na mabadiliko watatoa taarifa ili Serikali ichukue tahadhari.
    Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba alisema mkutano huo unahusu mashirika ya hali ya hewa kutoka nchi za pembe za Afrika kujadili msimu wa mvua utakaoanza Septemba hadi Desemba mwaka huu.
    Dk Tizeba alisema watazishauri Serikali za nchi husika kuchukua tahadhari kwenye mamlaka za miji kuhusiana na mvua hizo.
    Alisema mabadiliko ya hali ya hewa yatagusa kwenye sekta ya miundombinu na kilimo, hivyo Serikali itajipanga kuchukua hatua.
    "Tunasubiri majadiliano ya wataalamu wa hali ya hewa yanayofanyika siku mbili watuambie cha kutufanya," alisema Dk Tizeba.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.