May 21, 2014

  • Waziri huyu kalidanganya Bunge ni hatari sana

    Nipo hapa nikisikiliza hotuba ya Bajeti ya wizara ya Ujenzi inayosomwa na Waziri John Magufuli. katika hotuba yake ameliambia Bunge sasa hivi kuwa UJENZI WA BARABARA YA LAMI KUANZIA TABATA DAMPO HADI KIGOGO UNAENDELEA.

    Jamani mimi ni mtumiaji wa kila siku wa barabara hii ya Tabata Dampo Kigogo nikitokea Tabata Segerea kuelekea Mjini kwenye shughuli zangu. Mara ya mwisho nimepita leo hii jioni. ukweli ni kwamba WAZIRI AMELIDANGANYA BUNGE na hakuna hata dalili za kuwepo kwa ujenzi wa barabara ya lami zaidi ya kuharibika vibaya kwa barabara hiyo.

    Nawaomba wabunge wa dar es salaam kusimama kidete kupinga uongo huu wa Magufuli ambao hauna faida kwa wananchi. Mnyika na Mbunge wa Kinondoni Idd Azan tafadhalini hakikisheni mnamwambia ukweli Magufuli kuwa amewadanganya wananchi na taifa lote kwa ujumba.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.