May 21, 2014

  • Daima ukisema ukweli Tanzania jua maisha yako yapo hatarini

    Hivi inaweza kuwa kweli? Ukimjumlisha na huyu bwana wa EWURA Wazalendo na Wasema Kweli Wataisha.
     
    Kifo cha Mgimwa kiliingia kwenye mlolongo
    wa vifo kadhaa vyenye utata vilivyowahi
    kutokea nchini katika kipindi cha miaka 20
    iliyopita.
    Mawaziri wawili waliopata kuongoza Wizara
    ya Fedha nao wanadaiwa kufa katika
    mazingira ya kutatanisha, miongoni mwao
    akiwa Profesa Kighoma Ally Malima aliyekufa
    Julai 16, 1995.
    Alipojiengua CCM na kuhamia NAREA (NRA),
    Prof Kighoma alikwenda Makka katika hijja
    ya UMRA. Kabla ya kwenda kwake huko
    aliahidi pindi atakaporudi Tanzania atakuja
    kutoa yaliyopo moyoni mwake. Baada ya
    kumaliza hijja alielekea Uingereza na mauti
    yakamkuta huko.
    Ilienea katika kila kona ya Tanzania kuwa
    inawezekana kuna FITNA iliyosababisha kifo
    chake japokuwa wengine wanasema hakuna
    FITNA yoyote.
    Steven Kibona, aliyepata kuwa Waziri wa
    Fedha enzi za Alhaj Ali Hassan Mwinyi,
    pamoja na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu,
    Gilman Rutihinda, nao walikufa vifo vya
    utata.
    Kuna taarifa zilizodai kwamba, wazalendo
    hao walikataa kuchapisha fedha na
    kuziingiza kwenye mfumo kwa kutambua
    kwamba kufanya hivyo kungeongeza
    mfumuko wa bei na ugumu wa maisha
    ungeongezeka.
    Kibona alipelekwa na aliporejea huko
    akaanza kuumwa. Ikaelezwa kwamba
    amekula vyakula vya Kihindi ndiyo maana
    alikumbwa na tumbo la kuhara kwa sababu
    ya ugeni wa chakula. Hakukaa muda mrefu
    akafariki dunia.
    Rutihinda naye alipata ajali asubuhi tu akiwa
    anatoka nyumbani kwake. Taarifa
    zilizokuwepo ni kwamba ilikuwa ajali ya
    kawaida!
    Mwingine ambaye kifo chake kina utata ni
    Horace Kolimba. Huyu anajulikana kwa kauli
    yake aliyoitoa kwamba CCM haikuwa na dira
    wala mwelekeo. Akaitwa Dodoma 'kuhojiwa'.
    Lakini Machi 15, 1997 majira ya saa 11 jioni
    wakati akijiandaa kutoa maelezo yake,
    akadondoka ghafla. Walipompeleka hospitali
    ya Mkoa wa Dodoma tayari alikuwa 'wa
    jana'.
    Hivi, hakuna anayeweza kutoa taarifa rasmi
    kuhusiana na vifo hivi vyenye utata au kifo
    cha kiongozi yeyote kinapotokea mpaka
    tusubiri 'redio mbao'?
    Nawasilisha.
     
    Source:By Babalao 2 Via JF
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.