Watu watatu wanaodhaniwa
kuwa ni majambazi waliohusika na utekaji na unyan'ganyi wa gari Mei 12 mwaka huu
eneo la Mlima Msangamwelu Wilaya ya Mbeya Vijini wameuawa na wananchi katika
mapambano makali pembezoni mwa Mlima Mbeya.
Jambazi la
kwanza lilitambuliwa kwa jina la Kitwana Lugoya(30)mkazi wa Ilemi Juhudi Jijini
Mbeya ambaye aliuwa na wananchi baada ya kupata taarifa ambapo walifanikwa
kumzingira na kufanikiwa kumkamata eneo la Msangamwelu Kata ya Mshewe.
Juhudi za wananchi
ziliendelea kwa kushirikiana na Jeshi la kuwasaka majambazi wengine ziliendelea
na kufanikiwa kuwakamata majambazi wengine wawili waliotambuliwa kwa majina ya
Ndayobi Lutego(26)mkazi wa Igunga mkoani Tabora na Idd Sadiki(29) mkazi wa Veta
Jijini Mbeya.
Hata hivyo juhudi za
wananchi ziliendelea kuwasaka majambazi wengine wawili waliosalia wakiwa na
bunduki na risasi kadhaa ambao walitokomea katika msitu mnene kupandisha Mlima
Mbeya na kufanikiwa kukamata jambazi jingine lililokuwa na silaha na mfuko wa
risasi ambapo wananchi walilidhibiti ndipo alirusha silaha na risasi msituni na
kuanza kupambana na wananchi kwa kusaidiana na Askari na kufanikiwa kumkamata na
katika mapambano hayo jambazi hilo liliuawa kwa kutumia silaha za jadi na mawe.
Jambazi mwingine
alikamatiwa katika Kitongoji cha Lunji Kijiji cha Ihombe kwa ushirikiano na
wananchi wa vijiji vya Ihombe,Iziwa,Ikukwa na Msangamwelu ambalo pia lilipambana
na wananchi hao na Askari majira ya saa tano asubuhi Mei 13 mwaka huu ambapo
lildhibitiwa na kuuawa.
Mapambano hayo ya hatari
katika msitu huo yalikuwa yakifanyika kwa tahadhari kubwa kutokana na kutojua
idadi yao na aina ya silaha walizo nazo na mpaka sasa silaha na risasi
havijapatikana katika msitu huo.
Baadhi ya majambazi kabla
ya kuuawa imedaiwa kujihusisha na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha katika
mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Njombe,Iringa na Morogoro ambapo walikuwa
wakitafutwa kwa muda mrefu na Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi
limewashukuru wananchi waliojitolea kupambana na majambazi hao kwa kutumia dhana
ya Polisi Jamii na ulinzi shirikishi ambayo imeanza kuzaa matunda na kufanikiwa
kukomesha vitendo vya uhalifu Mkoani Mbeya ili Mbeya iwe na amani muda wote.
Wakati wa uporaji
majambazi hayo yapatayo matano yalipanga mawe barabarani eneo la Msangamwelu na
kufanikiwa kupora pesa,simu na pikipiki aina ya SANYA yenye namba T 682 CHT
ambayo baadaye waliitelekeza msituni walipokuwa wanafuatiliwa na wananchi.
Majambazi hao walimjeruhi
Dereva wa roli hilo aliyefahamika kwa jina la Sephen Mgogo ambaye amelazwa
katika Hospitali Teule ya Ifisi na miili ya majambazi hao imehifadhiwa katika
Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya ambapo wawili kati yao hawajatambuliwa.
Jeshi la Polisi
waliondoka Kijiji cha Ihombe majira ya saa moja na nusu usiku baada kazi ngumu
ya kubeba miili ya majambazi hao mwendo wa masaa matano kwa miguu kutoka uneo la
mapambano.
Na Ezekiel
Kamanga
wa Mbeya
yetu
|
0 comments:
Post a Comment