May 22, 2014

  • MFANYAKAZI WA BILIONEA WA IPP AFUNGUKA LIKE NEVER BEFORE SOMA ALICHOSEMA KUHUSU BOSI WAKE WA ZAMANI!!

     
     
     
     

    REGINALD Mengi ni mtu ambaye anapenda sana kujionesha mbele ya jamii kama mtu mwema na muungwana, lakini kwa wanaomfahamu kwa undani wanasema hana uadilifu ambao anataka kuiaminisha jamii kwamba anao.


    Ni mtu mwenye hila, anayependa uhasama na mkatili sana asiye na huruma hata kidogo. Hapa chini ni maelezo mafupi ya mwenendo wa mtu huyu ambaye sasa anapenda kuitwa Dakta Mengi (hulazimisha vyombo vyake vya habari kumuita hivyo), wakati hana elimu ya udaktari wa falsafa.
    CHUKI NA FITINA
    Mengi ni mtu anayependa sana kuanzisha chokochoko na watu ambao anaamini wanakwamisha masilahi yake binafsi. Mifano ya chokochoko alizozianzisha ni mingi na hakuna haja ya kuirudia yote. Lakini huwezi kuzungumzia fitina na chokochoko na mtu huyu bila kutaja suala la ununuzi wa Hoteli ya Kilimanjaro ambapo yeye alikuwa mmoja wa 'bidders' lakini alienguliwa baada ya kubainika kwamba hana uwezo. Alianzisha fitina na aliyekuwa Waziri katika Ofisi ya Rais wakati huo, Wilson Masilingi, akimtuhumu kuwa ndiye aliyehusika katika kile alichokiita 'mchezo mchafu' uliosababisha yeye kukosa zabuni ya kuinunua Hoteli ya Kilimanjaro. Alivitumia sana vyombo vyake vya habari kuandika uzushi mwingi kuhusu mchakato wa ununuzi wa Hoteli ya Kilimanjaro Alionesha pia chuki za waziwazi dhidi ya Rais wa wakati huo Benjamin Mkapa akidai ndiye aliyemuengua katika mchakato huo. Mwaka 2005 alianzisha gazeti la THISDAY kwa lengo la kuandika habari za uchunguzi. Lakini taarifa za watu wake wa karibu zinasema madhumuni makuu ya kuanzisha gazeti hilo yalikuwa ni kupambana na wabaya wake, akiwemo Rais Mkapa. Gazeti hilo liliandika mambo mengi mabaya dhidi ya Rais Mkapa huku yeye akitamba kwamba anamkomesha 'mbaya wake'. Kuna ushahidi kwamba yeye ndiye aliyekuwa anahangaika kupata baadhi ya nyaraka muhimu na kuwapa wahariri wake ili wamwandike vibaya Rais Mkapa.
    Alichokifanya wakati huo ndicho anachokifanya sasa pia dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo. Baada ya Prof. Muhongo kumuumbua, tena kupitia Televisheni yake mwenyewe wakati wa Mdahalo wa Chuo Kikuu mwishoni mwa 2013, kwamba katika suala la vitalu vya gesi hana uchungu na wafanyabiashara wazalendo bali ni mbinafsi, amejenga chuki za waziwazi dhidi ya waziri na wizara kwa ujumla. Hutumia mtandao wake wa wahariri wa magazeti mbalimbali kumchafua waziri na wizara kwa ujumla. Mmoja wa wahariri, Martin Malera wa gazeti la Tanzania Daima, amekiri jinsi anavyopewa fedha nyingi kwa kuandika habari mbaya dhidi ya Waziri Muhongo. Vyombo vyake vya habari vina maelekezo maalum kuhusu jinsi ya kumchafua Muhongo kwa kufuatilia kwa karibu mambo yake yote. Ushahidi wa hili ni aina ya habari 'negative' dhidi ya Prof. Muhongo zinazoandikwa na kutangazwa na vyombo vyake vya habari. Mmoja wa wahariri wa magazeti yake anaeleza kuchukizwa kwake na shinikizo la kuandika habari mbaya dhidi ya Prof. Muhongo.
    Mengi amekuwa akifanya hivyo kwa 'wabaya' wake wote, na mara nyingi hutoa maagizo ya kutoandikwa kabisa kwa habari za baadhi yao. Amefanya hivyo kwa akina Rostam Aziz, Yusuf Manji na Edward Lowassa. Hata hivyo, mmoja wa wabaya wake hao ndiye aliyem-blackmail kwa kuchukua picha zake za ufuska akiwa na binti mmoja hotelini nje ya nchi. Umafia huo ulimfanya amuangukie huyo bwana na sasa kwa unafiki mkubwa anajifanya ni rafiki yake, na anamwandika vizuri kwenye vyombo vyake vya habari.


    DHULUMA KWA WAFANYAKAZI/TUHUMA ZA MAUAJI
    Mtu huyu anatuhumiwa kuwatumia askari wa zamani waliofukuzwa jeshi la polisi kwa kukosa uadilifu – Nyanda na Ngaiza- ili kujaribu kumuangamiza kwa sumu mmoja wa wasaidizi wake wa karibu aitwaye John Marandu, ambaye hata hivyo alinusurika. Jalada la kesi hii lilifunguliwa Kituo cha Polisi Oysterbay na linaweza kupatikana pale. Kisa kilianza baada ya Marandu kuacha kazi na kuanza kudai masilahi yake. Lakini pia alikuwa na hofu kuwa Marandu, aliyekuwa personal assistant wake kwa upande wa media, angeweza kufichua maovu yake mengi. Suala hili limefichwa sana kwa nguvu ya fedha lakini gazeti moja liliwahi kuandika kwa undani taarifa hizi (Gazeti litaambatanishwa). Msaidizi wake mwingine aliyekuwepo kabla ya Marandu, aitwaye Lucas Liganga, pia aliacha kazi kwa Mengi baada ya kutoridhishwa na mwenendo wake. Huyu amejenga chuki mbaya sana dhidi ya Mengi!
    Tukio hilo limewafanya wafanyakazi wengine wanaodai haki zao baada ya kuacha kazi kusita kufuatilia kwa hofu ya kudhuriwa.
    Kwa muda mrefu, Mengi amekuwa akifanya jitihada za kuwapata waandishi wa habari wazuri kutoka vyombo vingine kwa ahadi ya kuwalipa vizuri zaidi lakini huishia kuwatapeli kwa kutowalipa fedha zao. Aliwahi kuchukua waandishi na wahariri kutoka Daily News na Mwananchi Communications lakini karibu wote walitimka kutokana na usanii na ubabaishaji wake, hasa katika suala la maslahi. Huyu ni mtu ambaye ameua career za waandishi wa habari wengi ambao wameichukia tasnia ya habari kutokana na uovu waliofanyiwa na Mengi.
    Mpaka sasa kuna waandishi wa habari wengi wameacha kazi ya uandishi wa habari au kuhamia vyombo vingine vya habari kwa sababu ya 'frustrations' kutoka kwa Mengi, na bado hajawalipa malimbikizo ya mishahara yao. Kuna orodha ndefu ya waandishi wa habari waliowahi kufanya kazi kwa Mengi na kuondoka kwa sababu yake. Lakini katika orodha hiyo wamo ambao walifariki dunia kutokana na mateso yaliyosababishwa na mtu huyu.
    REGINALD MHANGO – Mwandishi na mhariri makini aliyefanya kazi kwa muda mrefu katika magazeti ya serikali, Daily News na Sunday News hivi sasa ni marehemu. Lakini taarifa zinaonesha kuwa Mhango alifariki kutokana na matatizo yaliyosababishwa na Mengi, baada ya kumtelekeza, licha ya umahiri wake. Mhango alifanya kazi kwenye magazeti ya Mengi kwa awamu mbili; mara ya kwanza aliacha kazi na kurejea kwao Malawi, lakini Mengi alimshawishi arudi tena licha ya kwamba kule Malawi alikwishapata kazi nzuri. Aliachana naye muda mfupi, tena huku akiwa mgonjwa na kusababisha kifo chake.

    VUMI URASSA- Huyu alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa The Guardian Limited. Hivi sasa ni marehemu, na ndugu zake wanamshutumu Mengi kwa kifo chake kwani ndiye aliyem-frustrate licha ya kumtumikia kwa uaminifu kwa muda mrefu kama mkurugenzi. Alimwachisha kazi bila sababu maalum, na ndipo alipoanza kuumwa hadi mauti ilipomkuta. Mengi alishindwa hata kuhudhuria shughuli ya msiba wa Urassa licha ya kwamba wanatoka sehemu moja huko Machame, Kilimanjaro na wana uhusiano wa kifamilia. Alituma salamu na kujifanya ameshindwa kuhudhuria mazishi wakati alikuwepo Dar es Salaam.
    OMARI MROPE – Huyu ni marehemu ambaye alikuwa 'victim' wa ukatili wa Mengi. Mwaka 2010 akishirikiana na Mkurugenzi wa The Guardian, Kiondo Mshana, aliamuru kuhamishiwa mikoani na wilayani (tena kusiko na ofisi) waandishi wa habari na wafanyakazi wote aliowachukia kwa sababu mbalimbali. Mrope alikuwa mmoja wapo na alitupwa kwenye moja ya wilaya zisizo na ofisi wala vitendea kazi. Alikufa kwa frustrations!
    Waandishi na wahariri wengine walilazimika kuacha kazi na kujikita katika taaluma nyingine walizosomea. Miongoni mwa hawa wamo wanasheria JUMA THOMAS na NYARONYO KICHEERE. Huyu Kicheere alimchukua kutoka The Citizen na kumfanya mhariri wa gazeti la Kulikoni, lakini baadaye akamhamishia The Guardian na kum-frustrate, ikiwa ni pamoja na kutomlipa mshahara wake stahiki. Wengine ni EVARIST MWITUMBA aliyekuwa mhariri mtendaji wa THISDAY na BOB KARASHANI ambao wameamuza kujitegemea kwa kufanya shughuli zao kama Media Consultants. Hawa nao inasemekana bado wanadai malimbikizo ya mishahara yao na Mengi hajaonesha nia ya kutaka kuwalipa.
    Kuna orodha ndefu ya waandishi wengine vijana ambao hata hivyo waliamua kutimkia kwenye vyombo vingine vinavyojali utu. (Orodha yao na kiwango cha pesa wanachodai itapatikana).
    KUTOKOPESHEKA KWA KAMPUNI ZAKE
    Wafanyakazi wa kampuni na mashirika mbalimbali hupata mikopo kutoka kwenye taasisi mbalimbali za kifedha lakini IPP ni miongoni mwa kampuni zilizokuwa 'blacklisted' kwa sababu ya kukosa uaminifu katika kulipa. Lakini hii kwa kiasi kikubwa inatokana na kampuni zake nyingi kutokuwa na uhakika wa mishahara. Wakopeshaji wanaoitwa TUNAKOPESHA LIMITED wamepiga marufuku kukopeshwa kwa wafanyakazi wote wa kampuni za Mengi kwa sababu ya ubabaishaji katika malipo. Benki kadhaa ikiwemo Barclays hazitoi tena mikopo kwa kampuni za mtu huyu.
    KESI YA UINGEREZA
    Alipata hasara kubwa mwaka 2012 pale alipofungua kesi dhidi ya raia wa Uingereza Sarah Hermitage kwa madai ya kukashifiwa. Alishindwa vibaya kesi hiyo na kulipa mamilioni ya paundi. Alitumia nguvu kubwa kuzuia kuandikwa kwa habari za kushindwa kwake kwenye kesi, lakini hukumu ya kesi inaambatanishwa hapa. Angalia jinsi Jaji wa Uingereza alivyomuona kuwa ni mshiriki wa corruption na mtu asiyetaka kuguswa.
    HUYU NDIYE MTU ANAYETAKA KUUAMINISHA UMMA KUWA NI MTU SAFI WAKATI NI KATILI MKUBWA ASIYE NA HURUMA.

    Ndimi, aliyekuwa mfanyakazi wa IPP.

  • 1 comments:

    1. Umetumwa we we onesha ushaidi sio unaandika kwa kusikia kwa watu..unaonekana kabisa unavhuki naye jipange

      ReplyDelete

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.