May 10, 2014

  • MASTER J ASHAURIWA NA MAMA YAKE KUMTAMBULISHA RASMI SHAA KAMA MPENZI WAKE

     
     
     

    Ni miaka mingi sasa imepita toka ifahamike kuwa CEO wa MJ Records Joachim Kimaryo aka Master J na mwimbaji Sarah Kaisi aka Shaa ni wapenzi, kiasi mpaka sasa hata wanapoulizwa kwenye interviews na mitandao ya kijamii hukiri kuwa wao ni couple.
    Lakini mama mzazi wa Master J ameona kuna haja ya mwanae kuuweka wazi rasmi uhusiano wao ili jamii iwe na taarifa sahihi, hivyo amemshauri mwanaye kuwaita waandishi wa habari kuzungumzia uhusiano wao na mipango yao ya 'ndoa'.
    "Hili ni jambo ambalo kusema kweli limekuwa kubwa sana sasa hivi," Alisema MJ kupitia E-News ya EATV. "Nilikuwa nimekaa na mama yangu mzazi amenishauri ameniambia sikiliza uite watu wa media wewe na huyo Sarah muwe open kwa sababu kiukweli mnavyoendelea kukaa kimya kila mtu anakuwa ana assume mambo yake ambayo mwisho wa siku yanaweza kuleta madhara flani".

    Mj ambaye ni baba wa watoto watatu ameahidi kuwaita waandishi wa habari mwaka huu ili kumtambulisha rasmi Shaa kama mpenzi wake na mipango yao ya baadaye.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.