May 26, 2014

  • Kajala Akiwa Street Bila Make Up, Agoma Kupigwa Picha




    Kajala Akiwa Street Bila Make Up, Agoma Kupigwa Picha
    MASTAA wetu Bongo ukimtokea ghafla na ukataka kumpiga picha bila kujiremba unaweza kumuua kwa hofu, siku za karibuni kamera ya FC ilimkosesha raha nyota wa filamu Swahiliwood Kajala Masanja pale alipokutana na mpiga picha wetu na kutaka kumpiga picha kama sehemu ya kumbukumbu katika matukio, msanii huyo alizuia huku akilalamika.
    "Aaah sitaki jamanii unanipigaji picha hivi hata sijajiandaa jamani, nipo rafu sipendi ukipiga picha angalau uwe smart, usinipige picha sitaki sitaki sijajiandaa picha zitakuwa mbaya please usifanye hivyo,"anasema.
    Utafiti unaonyesha kuwa mara nyingi nyota wa filamu wamejenga tabia ya kujiandaa kwa kujipodoa wakiwa wapo location au wakifanya mahojiano na wanahabari, hivyo kuwa na muonekano tofauti na wanavyokuwa na isha ya kawaida wakiwa katika mishemishe zao

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.