May 26, 2014

  • HESLB WASEMA :Vyuo vilivyokamilisha taratibu vimeshapelekewa fedha za mikopo



    HESLB WASEMA :Vyuo vilivyokamilisha taratibu vimeshapelekewa fedha za mikopo
    Mkurugenzi wa Habari,Elimu na Mawasiliano wa HELSB, Cosmas Mwaisobwa
    Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imesema kwa kiwango kikubwa vyuo ambavyo vimetimiza vigezo, utaratibu wa kupata mikopo kwa ajili ya wanafunzi wake kwa mwaka 2014/15 umekamilika. 

    Kulikuwapo na madai kwamba fedha hizo zitachelewa kwa kuwa serikali  imepeleka fedha nyingi katika Bunge Maalum la Katiba.

    Akizumngumzia madai hayo, Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HELSB, Cosmas Mwaisobwa, alisema kuwa vyuo ambavyo havijapelekewa fedha muda wao wa kupelekewa bado.
    "Suala la kusema fedha zimeelekezwa katika Bunge la Katiba mimi siwezi kulizungumzia, kwa kuwa mimi siyo mwanasiasa," alisema Mwaisobwa na kuongeza:
    "Kwa vyuo ambavyo bado havijapata mkopo ni kutokana na kutofikia tarehe ya vyuo husika kupata mikopo. Kwa hiyo wasije wakatamani kwa kuona wenzao ambao tarehe yao ilifika mapema ya kupata mkopo, wasubiri na wao zamu yao itafika. Mfano, Chuo cha Tumaini wameshapata, lakini Chuo cha Ruaha bado."
    Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Musa Mdede, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema vyuo ambavyo tarehe ya kupata mkopo wameshapelekewa hundi kwa ajili ya kusainiwa ili wapatiwe fedha.
    "Nina taarifa za chuo cha SAUT cha Mwanza, UDSM, IFM, DIT naTumaini kwamba wameshapelekewa hundi na vingine ambavyo vipo Dar es Salaam. Na mara nyingi kuchelewa au kuwahi kufika kwa fedha za mkopo chuoni kunategemea zaidi ni lini chuo husika kinafunguliwa," alisema Mdede.
     
    CHANZO: NIPASHE


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.