May 25, 2014

  • KINANA AHITIMISHA MKUTANO WAKE WA HADHARA KWA KISHINDO MJINI SINGIDA

    Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi (hawapo pichani) kando kando ya barabara,wakati wakielekea kwenye mkutano hadhara unaonfanyika katika uwanja wa People's mjini Singida,akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye na viongozi wengine mbalimbali chama.
    Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi wakati akiwasili kwenye mkutano wa hadhara unaonfanyika katika uwanja wa People's mjini Singida jioni hii,akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Mwigulu Nchemba na viongozi wengine mbalimbali wa chama.
    Naibu Katibu Mkuu wa CCM,na Mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki,Mh Mwigulu Nchemba akiwa kwenye moja ya piki piki kwenye matembezi ya kuelekea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa People's mjini Singida,ambao wananchi wamejitokeza kwa wingi.


    Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa mji wa Singida jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja waPeople's mjini Singida.Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikad,siasa na Uenezi Nape Nnauye,wakiwa kwenye ziara ya siku nane mkoani humo ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
    Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa mji wa Singida jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa People's mjini Singida
    Sehemu ya Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara unaoendelea hivi sasa katika uwanja wa People's mjini Singida,
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.