June 17, 2014

  • NEWS ALERT: SHEKHE WA MKOA WA TABORA NA WAUMINI WATANO WAPANDISHWA KIZIMBANI



    NEWS ALERT: SHEKHE WA MKOA WA TABORA NA WAUMINI WATANO WAPANDISHWA KIZIMBANI
    Na Allan Ntana, Tabora 
     SHEKHE wa mkoa wa Tabora Salum Shaban Salum na waumini wenzake watano  wamefikishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mkoani hapa akikabiliwa na shitaka la kufanya fujo katika msikiti wa Ijumaa mkoani hapa. 
     Wakili wa serikali Juliana Changalawe akisoma mashitaka hayo mbele ya hakimu mfawidhi wa mkoa wa Tabora Issa Magoli alidai kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo mnamo tarehe 14 Juni 2014 katika msikiti mkuu wa Ijumaa uliopo eneo la Gongoni mjini hapa. 
     Wakili huyo aliiambia mahakama kuwa siku hiyo majira ya mchana watuhumiwa Shaban Salum, Mgude Ahmed, Said Maganga, Kassim Shomary, Abubbakar Ludenga na Kassim Rajab walimtoa katika ibada Shekhe Ibrahim Mavumbi. 
     Watuhumiwa ambao wanawakilishwa na wakili Mussa Kwikima wa mjini hapa mara baada ya kusomewa shitaka hilo wote walikana na kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 30/06/2014 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwani upelelezi umeisha kamilika na wote walipata dhamana.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.