Mratibu wa Shindano la kumtafuta mrembo wa Redd's Miss Chang'ombe, Tom Chilala (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo wakati wa kuitangaza zawadi za washindi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Marie Stopes, Dk. Jophn Bosco na Ofisa Uhusiano wa TV1, Mponjoli Katule.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Marie Stopes, Dk. Jophn Bosco akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo.
Rapa wa bendi ya Ruvu Stars, Msafiri Diouf 'Sokoine' akighani wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Warembo wakiwa wamepozi kwa picha.
MNYANGE atakayevishwa taji la Redds Miss Temeke 2014 linalotarajia kufanyika Juni 27 mwaka huu katika ukumbi wa TTC Chang'ombe anatarajia kujinyakuria kitita cha sh. laki tano.
Mshindi wa pili atajinyakulia laki tatu, mshindi wa tatu laki mbili na washiriki wengine watapata kifuta jasho cha sh. 65,000.
Mratibu wa shindano hilo Tom Chilala, alisema katika shindano hilo anatarajia kumtoa mrembo atakafanikiwa kutwaa taji la misi Tanzania mwaka huu hapo baadaye.
"Mwaka huu nina warembo wazuri na wenye vigezo vyote, naamini mwaka huu nitarudisha heshima yangu ya kufanikiwa kutoa warembo kutoka Redd's Miss Temeke hadi Redd's Miss Tanzania," alisema.
Alisema mwaka 2010 alifanikiwa kumtoa Genevieve Emmanuel, kutoka miss Temeke hadi miss Tanzania, hivyo na kwa mwaka huu anaamini itakuwa hivyo kutokana na warembo alionao.
Aidha shindano hilo litakarokuwa na washereheshaji kutoka bendi ya Ruvu Stars, Mchekeshaji Kitale pamoja na msanii anayetamba na kibao cha Basi Nenda Moshi Katena na wengine. Kiingilio katika shindano hilo kitakuwa ni sh. 20,000 kwa VIP na Elfu 10000 kawaida.
Naye Mkurugenzi wa Marie Stoper John Bosco ambao ni wadhamini wa shindano hilo alisema wameamua kudhamini mashindano hayo kwa lengo la kuwaelimisha vijana kuhusiana na uzazi wa mpango.
Alisema hawataishia hapo wanaendelea kudhamini hadi miss Tanzania kutokana na kuona vijana hao wanaweza kuliwakilisha taifa."Katika sensa viijana ndio wameonekana kuwa na asilimia kubwa hivyo ni vizuri kuwa dhamini ili kuweza kujenga kizazi ambacho kimewezeshwa ambacho hakitaweza kuwa taifa tegemezi," alisema.
0 comments:
Post a Comment