June 27, 2014

  • ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WA CHINA ENEO LA MAMLAKA YA UKANDA MAALUM WA UWEKEZAJI NCHINI (EPZA)



    ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WA CHINA ENEO LA MAMLAKA YA UKANDA MAALUM WA UWEKEZAJI NCHINI (EPZA)
    EPZA 1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Tooku Garments CO.LTD katika eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji nchini (EPZA) wakati alipotembelea kiwanda hicho mapema jana jijini Dar es Salaam, kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda.
    EPZA 3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao (wapili toka kushoto) akikagua bidhaa za nguo zinazozalishwa na kiwanda cha nguo cha Tooku Garments CO.LTD. katika eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji nchini (EPZA)wakati akihitimisha ziara yake mapema jana jijini Dar es Salaam, wa tatu toka kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda.
    EPZA 4Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao akizungumza na mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Tooku Garments CO.LTD katika eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji nchini (EPZA)wakati akihitimisha ziara yake mapema jana jijini Dar es Salaam
    EPZA 5Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiangalia moja ya nguo zinazotengenezwa na kiwanda cha nguo cha Tooku Garments CO.LTD katika eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji nchini (EPZA) wakati wa kukamilisha ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao mapema jana jijini Dar es Salaam.
    EPZA 6Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdalah Kigoda (kushoto) akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao wakati alipotembelea kiwanda cha nguo cha Tooku Garments CO.LTD katika eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji nchini (EPZA)akihitimisha ziara yake nchini mapema jana jijini Dar es Salaam.
    Picha zote na Eliphace Marwa – MAELEZO


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.