June 30, 2014

  • SHUKRANI: TEAM LIBE FOR DMV COMMUNITY PRESIDENT 2014


    SHUKRANI: TEAM LIBE FOR DMV COMMUNITY PRESIDENT 2014
    Liberatus "Libe"
     mgombea nafasi ya Urais

    Team Libe for DMV Community President 2014 tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa kila mmoja aliye weza kufika kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara jana Meadowbroak Park. Pia tunapenda kuwashukuru wale walio kuwa na nia ya kuja lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao wakashindwa kutimiza hadhma hiyo.  Asanteni!

    Pia, Team Libe for DMV Community President 2014 tunapenda kuwashukuru wagombea wengine kwa kujitokeza na kuonyesha ushirikiano chanya na kufurahia mazungumzo na wapiga kura; asante mama Salma Manyoka/mgombea makamu wa Rais, asante Heriet Shangarai/ mgombea makamu wa Rais, asante Solomon Cris/mgombea makamu wa katibu
     
    Mama Salma/Mgombea makamu wa Rais
    Zaidi, shukrani zetu za dhati zinaenda kwa Ndg. Hamza Mwamoyo/Mwenyekiti wa board, Mzee Safari/ Mkiti wa tume ya uchaguzi na mke wake mama Safari, kaka yetu Jabil  Jongo/ mjumbe tume ya uchaguzi na mchungaji Malekela kwa kuonyesha mapenzi yasio na ukomo kwa jumuia yetu ya DMV.
     
    Heried Shangarai/Mgombea makamu wa Rais
    Mwisho, tunawashukuru wana DMV wote kwa kuwa na ushirikiano thabiti na kusaidiana kwenye raha na shida. Kama imani ya kimsingi ya ", Team Libe for DMV Community President 2014"inavyo sema "binadamu tupo hapa ili tushirikiane na sio kushindana wala kutengana."
    Solomon Cris/Mgombea makamu wa katibu

    Team Libe for DMV Community President 2014 
    wishes all Muslims Ramadan Kareem.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.