June 26, 2014

  • Balozi mpya wa Marekani nchini amtembelea Waziri Muhongo

     
     
     
     
    Na Veronica Simba
    Balozi mpya wa Marekani hapa nchini Mhe. Mark Childress leo ametembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Waziri mwenye dhamana, Profesa Sospeter Muhongo.

    Katika mazungumzo yao, Balozi Childress aliyeambatana na Ujumbe wake ameahidi nchi yake kuimarisha ushirikiano na Tanzania kwa kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo hususan katika sekta ya gesi asilia.

    Awali, Profesa Muhongo alimweleza Balozi Childress fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini hususan katika sekta za nishati na madini na kuweka bayana dhamira ya dhati ya Serikali kuinua uchumi wa nchi kupitia sekta husika.
    Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Mark Childress akimweleza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo utayari wa nchi yake kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hususan katika sekta ya gesi asilia. Balozi Childress na ujumbe wake leo wametembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam ambapo walikutana na kuzungumza na Waziri Muhongo na Maafisa Waandamizi wa Wizara pamoja na Taasisi zilizo chini yake.
    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Maafisa Waandamizi wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake, wakiwa katika mazungumzo na Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress na Ujumbe wake.
    Sehemu ya Ujumbe ulioambatana na Mhe. Balozi Childress, wakifuatilia mazungumzo baina ya Balozi huyo na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
    Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zilizo chini yake wakifuatilia kwa makini mazungumzo baina ya Waziri Muhongo na Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress aliyetembelea Wizarani leo akiwa na Ujumbe wake.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.